BUKOBA SPORTS

Sunday, May 5, 2013

SIR ALEX FERGUSON KUTOUONA MSIMU MPYA KWA SABABU ZA UPASUAJI.

Sir Alex Ferguson, huenda akaukosa mwanzo wa Msimu mpya wa Ligi ya BPL, Barclays Premier League, akitarajiwa kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha Mifupa ya Pajani mwishoni mwa Mwezi Julai.
Inadaiwa kuwa Opereshini hiyo, ambayo imethibitishwa na Klabu ya Man United, itafanywa mara baada ya Ziara ya Kabla Msimu mpya kuanza ambayo watatembelea huko Nchini Thailand, Australia, Japan na Hong Kong kwa Wiki 3.


Man United wanatarajiwa kucheza Mechi ya Fungua Pazia ya Msimu mpya wa 2013/14 Uwanjani Wembley hapo Agosti 11 kugombea Ngao ya Hisani dhidi ya Bingwa wa FA CUP ambae atakuwa Man City au Wigan ambao watacheza Fainali ya FA CUP hapo Mei 11.

Msimu mpya wa BPL wa 2023/14 utaanza Wikiendi ya Agosti 17 ambapo Man United wataanza utetezi wa Taji lao.

Mbali ya kuugua Miezi 12 iliyopita alipopatwa na matatizo ya kutoka damu puani, Ferguson, mwenye Miaka 71, amekuwa na afya njema na Msimu huu ameiongoza Man United kutwaa Taji lao la 20 la Ubingwa wa England hilo likiwa Taji lake la 13 la Ligi tangu atue Man United Novemba 1986.

Jana, wakiwa kwenye Kituo cha Man United cha Mazoezi huko Carrington, Ferguson aliwaalika Wanahabari kunywa Champagne ikiwa ni kusherekea ushindi wa Taji lao la 13 la Ligi Kuu.


Pia Ferguson yupo kwenye mipango ya hatua za mwisho kuchukua strika Radamel Falcao kuja Old Trafford kwa msimu huu unaokuja.

No comments:

Post a Comment