Saturday, December 21, 2013

HAWA NDIO NYOTA WANAOHAMA VILABU VYAO KWENYE DIRISHA DOGO ULAYA, WAPO LEWANDOWSKI, PIRLO, VALDES NA DIEGO


Main man: Robert Lewandowski (kushoto) anaweza kuondoka Borussia Dortmund na kujiunga na Bayern Munich
Zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya kufika mwezi Januari ambao kimsingi dirisha dogo la usajili litakuwa likifunguliwa.

Hebu tuangazie kwa pamoja tupate kujua wachezaji nyota kumi barani Ulaya ambao watakuwa nje ya mikataba wakati wa kiangazi na akina nani ambao watakuwa wako tayari kukatisha viporo vya mikataba yao kwa makubaliano ya fidia.


Robert Lewandowski

Mshambuliaji mwenye umri w miaka 25 wa Borussia Dortmund
Mshambuliaji huyu raia wa Poland ni mmoja kati ya kifaa cha nguvu katika soka, anatarajiwa kuweka wazi nini mipango yake ya baadaye mwezi Januari utakapo wadia.


Inaarifiwa kuwa Bayern Munich ndio eneo ambalo hasa mshambuliaji ataelekea lakini usiache kuvitazama vilabu kadhaa vya Barclays Premier League ambavyo vinapiga hatua kuelekea kupata huduma yake.

Arsenal, Chelsea na Manchester United vyote vimeonyesha nia huku Real Madrid pia inaonekana kumnyemelea.

Xabi Alonzo kiungo wa Reala Madrid mwenye umri wa miaka 32

Kiungo huyo wa zamani wa Liverpool kuna taarifa kuwa huenda karejea katika klabu yake ya zamani, ingawa kuna taarifa ya watu wenye majina nchini humo kugomea hilo nchini Hispania. Mashabiki wa Real Mdrid wanataka aendelee kusalia na katika kulithibitisha hilo wamekuwa wakimuunga mkono katika michezo ya hivi karibuni. Pia kuna taarifa nchini Hispania kuwa Jose Mourinho huenda akamchukua na kujiunga na Chelsea.


Maestro: Xabi Alonso

Andrea Pirlo mwenye miaka 34, kiungo Juventus

Ni zaidi ya habari kuwa Pirlo, mmoja kati ya wachezaji wenye heshima kubwa mchezoni atasaini mkataba wa kuongeza muda ndani ya klabu yake ya Juventus mwezi January.
Klabu hiyo ya nchini Italia haina wasiwasi na juu ya mpango huo mpya kwa Pirlo na kwamba litakuwa ni jambo bora.
Hata bado anaendelea kufukuziwa na vilabu mbalimbali Ulaya na hilo ni jaribio kubwa na swali kubwa ni nini kitatokea mwezi Januari.
Kiungo wa Italia na Juventus maestro Andrea Pirlo (kulia) akipambana na mchezaji wa Fiorentina Borja Valero

Bafetimbi Gomis umri wa miaka 28 Lyon

Swali ni je mshambuliaji huyu mfaransa ataondoka na kuelekea kucheza soka nchini England?

Wakala wake anasema huko hasa ndiko anakokutana kuelekea. Newcastle tayari wameonyesha nia kwake. Ilikuwa kidogo wafanikiwe kumsajili wakati wa majira ya kiangazi lakini ilishindikana kutokana na kutokukubaliana juu ya suala la mshahara.
Cardiff na Swansea pia wanapiga hatua kumnasa


Mshambuliaji mfaransa Bafetimbi Gomis anataka kuondoka Lyon

Jeremy Menez , 26, Paris Saint- Germain

Uwezekano wa mshambuliaji huyo wa kifaransa kuondoka linaonekana kama ni jambo jepesi kwa vilabu kadhaa vya Ulaya na wengi wakionyesha nia. Amekuwa akihusishwa na kutaka kuelekea Liverpool, lakini huenda wakakutana na upinzani kutoka katika vilabu vya Inter Milan, Roma na Juventus. Anaonekana kama anataka kuondoka ingawa pia wanaonekana wanapata kumuongezea mkataba.


Jeremy Menez huenda akaongeza mkatabat Paris Saint-Germain

Victor Valdes ,31,mlinda mlango wa Barcelona

Mlinda mlango huyu amekuwa nje kwa kipindi cha karibu wiki sita akisumbuliwa na misuli na klabu yake ya Barcelona siku zinakwenda harijojo. Paris Saint-Germain inamtaka huku taarifa nyingine nchini Hispania zikiarifu kuwa Manchester City wako na mpango wa kumnasa. Hizo zinaweza zikawa ni taarifa mbaya kwa mlinda mlango namba moja wa England No 1 Joe Hart.


Victor Valdes

Diego,28, kiungo wa Wolfsburg.
Kiungo huyu mshambuliaji wa Ki-Brazil anakaribia kuondoka katika kikosi cha Wolfs kinachoshiriki ligi ya Ujerumani Bundesliga. Anataka kuelekea Premier League na amekuwa akieleza wazi kuwa anaipenda Arsenal au Southampton. Aina yake ya uchezaji inaonekana kufanana na pande zote mbili hizi ingawa bado vilabu hivyo havija onyesha wazi kuanza kumfuatilia.


Diego

Esteban Cambiasso, 33, kiungo wa Inter Milan

Huyu pia ni mchezaji mwenye umri wa kutosha ambaye ana mchango mkubwa katika kiungo na anaweza kuongeza uzoefu wake wa dimba la kati katika klabu yoyote ile duniani.

Inter inaarifiwa kuwa inamhitaji kuendelea kuwa naye, lakini suala la yeye kutaka kurejea nyumba ni linaonekana sio swali gumu tena kupatiwa majibu.


Esteban Cambiasso

Urby Emanuelson,27, kiungo wa AC Milan

Tayari ana uzoefu wa kutosha katika ligi kuu ya England wakiti akiwa na klabu ya Fulham kwa mkopo, ambako bosi wake wa zamani Martin Jol alichukizwa alipoona akiondoka kwa muda mfupi Kiungo huyu M-Dutch alikaririwa akisema anataka kucheza tena.


Urby Emanuelson

Wachezaji wa Primier League watakao kuwa nje ya mkataba majira ya kiangazi hawa chini
Nemanja Vidic, Samuel Eto’o, Bacary Sagna, Younes Kaboul, Patrice Evra, John Terry, Joleon Lescott, Ashley Cole, Frank Lampard, Rio Ferdinand

Blaise Matuidi, 26, kiungo wa PSG

Kuna tetesi kwamba Chelsea na Manchester City wanapanga miopango ya kuandaa 'pre-contract offers' kwa ajili ya Matuidi endapo itashindikana kukubaliana na masharti mapya na PSG. Kiungo huyo ana njia nyeupe ya kuelekea Premier League, lakini anasubiri kile ambacho kitawekwa mezani na klabu yake ya sasa.

Kajichokea: Blaise Matuidi huenda akaondoka PSG kama masharti mapya ya mkataba yatashindikana.

No comments:

Post a Comment