JOSE MOURINHO amedai kuwa Frank Lampard atarudi Chelsea kwa vile milango yote iko wazi kwake kutokana na amri ya Mmiliki wa Klabu Roman Abramovich.
Kwa mujibu wa Mourinho, Abramovich ameshatoa uamuzi kwamba Lampard akirudi apewe kazi yeyote anaechagua mwenyewe.Wiki iliyopita, Lampard alitangaza kuondoka Chelsea baada ya kuitumikia Miaka 13 na kuvunja Rekodi ya Mfungaji Bora kwa kupachika Bao 211 kwa Mechi 648 na pia kutwaa Ubingwa wa England mara 3, FA CUP 4, LIGI CUP 2, UEFA CHAMPIONS LIGI 1 na EUROPA LIGI 1.
Mourinho amegusia kwamba Lampard, ambae yuko na Kikosi cha England kinachokwenda kucheza Kombe la Dunia huko Brazil, uamuzi sahihi kwake ni kurudi Stamford Bridge na kuwa Meneja Msaidizi.
Mourinho ametoboa hilo lishakubalika kwa Abramovich na kusema: “Atarudi Chelsea. Mr Abramovich – Namba 1 hapa, Mtu muhimu hapa, anataka sana Frank awe hapa! Mie nataka awe hapa na kila Mtu anataka awe hapa! Hakika atarudi tu!”
Aliongeza: “Kitu kingine ni kuwa anaweza kurudi anavyotaka. Mista Abramovich ameacha Mlango wazi kabisa kwamba aje anavyotaka, afanye analotaka!”
Mourinho amesisitiza huu si mwisho wa Lampard kwa Chelsea bali ni mapumziko tu.
Inategemewa Lampard atakwenda kucheza Soka huko Marekani kwenye MLS na New York City lakini Msimu wao unaanza Machi 2015 na hivyo huenda akaamua kucheza Klabu ya England kungojea wakati huo na inadhaniwa huenda akachezea Klabu ya Mjomba wake, Harry Redknapp, huko QPR kwa Mkopo hadi ahamie huko Marekani.
Cesc Fabreagas njiani kutua Chelsea

No comments:
Post a Comment