ZIMEIBUKA habari kuwa UEFA imewaambia Wanachama wake kwamba haimuungi mkono Sepp Blatter kwenye azma yake ya kugombea Urais wa FIFA kwa mara ya 5 mfululizo.
Habari hizo zinadaiwa kuwataka Wanachama wa UEFA kutoshangilia wakati, kama inavyotegemewa, Blatter kutangaza kugombea tena Urais wa FIFA kwenye Kongresi ya FIFA itakayofanyika Wikiendi ijayo huko Sao Paolo Nchini Brazil wakati utakapofanyika Mkutano huo kabla Fainali za Kombe la Dunia kuanza huko Nchini Brazil hapo Juni 12.
Blatter, mwenye Miaka 78, ameshika wadhifa wa Urais wa FIFA tangu 1998 alipochaguliwa kwa mara ya kwanza na kuongoza kwa Vipindi Vinne mfululizo.
Uchaguzi mwingine wa FIFA ni Mwaka 2015.
Siku za nyuma, ilitegemewa Rais wa UEFA, Michel Platini, Staa wa zamani wa France, angeweza kugombea nafasi hiyo ya FIFA na inaaminika hata Sepp Blatter, wakati aliposhinda Uchaguzi wa 2011, alikubali kutogombea tena Urais Mwaka 2015 ili kumpisha Platini, lakini wengi wanaamini Platini hana nia tena kuwa Rais wa FIFA.

No comments:
Post a Comment