BUKOBA SPORTS

Thursday, June 5, 2014

VIWANGO NA UBORA WA SOKA DUNIANI: SPAIN BADO NI BALAA!! NI "NUMBER 1" GERMAN YA 2 IKIFUATIWA NA BRAZIL NAFASI YA TATU. TANZANIA NAYO YAJA KWA FUJO YAPANDA NAFASI 9 NI YA 113 KWA SASA.

WENYEJI wa Fainali za Kombe la Dunia, Brazil, wamepanda juu nafasi 1 na sasa wako Nafasi ya 3 katika Listi ya FIFA ya Ubora Duniani iliyotolewa Leo huku Mabingwa wa Dunia Spain wakibakia Nafasi ya 1, wakifuata Germany na Tanzania ikipanda Nafasi 9 na kukamata Nafasi ya 113.
England imerudi 10 Bora kwa kuishusha Greece wakati Argentina imepanda Nafasi 2 na ipo ya 5 na Uswisi ikoya 6 baada kupanda Nafasi 2.
Kwa Afrika, Timu ya juu kabisa ni Algeria iliyo Nafasi ya 22 baada kupanda Nafasi 3 na kuipiku Ivory Coast ambayo iko ya 23 baada kushuka Nafasi 2.


25 BORA:
1.        Spain [Iko pale pale]
2.        Germany [Iko pale pale]
3.        Brazil [Imepanda Nafasi 1]
4.        Portugal [Imeshuka Nafasi 1]
5.        Argentina [Imepanda Nafasi 2]
6.        Switzerland [Imepanda Nafasi 2]
7.        Uruguay [Imeshuka Nafasi 1]
8.        Colombia [Imeshuka Nafasi 3]
9.        Italy [Iko pale pale]
10.      England [Imepanda Nafasi 1]
11.      Belgium [Imepanda Nafasi 1]
12.      Greece [Imeshuka Nafasi 2]
13 USA [Imepanda Nafasi 1]
14 Chile [Imeshuka Nafasi 1]
15 Netherlands [Iko pale pale]
16 Ukraine[Imepanda Nafasi 1]
17 France [Imeshuka Nafasi 1]
18 Croatia [Imepanda Nafasi 2]
19 Russia [Imeshuka Nafasi 1]
20 Mexico [Imeshuka Nafasi 1]
21 Bosnia and Herzegovina [Imepanda Nafasi 4]
22 Algeria [Imepanda Nafasi 3]
23 Denmark [Iko pale pale]
23 Côte d'Ivoire [Imeshuka Nafasi 2]
25 Slovenia [Imepanda Nafasi 4]

TANZANIA-NAFASI ILIPO:
108 Kenya
109 Latvia
110 Bahrain
110 Canada
112 Niger
113 Tanzania [Imepanda Nafasi 9]
114 Namibia
115 Kuwait
116 Liberia
116 Rwanda

No comments:

Post a Comment