BUKOBA SPORTS

Saturday, June 7, 2014

WENYEJI BRAZIL WAIPIGA SERBIA BAO 1-0, MFUNGAJI NI FREDERICO GUEDES FRED ALIYEWAPA BAO HILO LA USHINDI.

Wenyeji wa Mashindano ya FIFA ya kuwania Kombe la Dunia, Brazil, waliwafunga Serbia Bao 1-0 huko Arena de São Paulo, au kwa Jina jingine Arena Corinthians.
Bao la Brazil lilifungwa katika Dakika ya 58 na Frederico Guedes Fred na kuwapa ushindi wao wa 15 katika Mechi 16 zilizopita.
Hulk aliifungia Brazil Bao safi lakini Refa Enrique Cáceres alilikataa kimakosa kwa madai ya Ofsaidi.
Alhamisi Brazil watacheza Mechi ya Ufunguzi ya Kombe la Dunia, wao wakiwa KUNDI A, dhidi ya Croatia.
Fred akitupia...
Neymar akimpa shida Mserbia Dusan Basta jana usiku,.......

Neymar akiwa na mchezaji anayekipiga kwenye Klabu ya Chelsea Ivanovic

Hulk dhidi ya mchezaji wa zamani wa Manchester United winga Zoran Tosic

Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari akimpa maelekezo mchezaji anayekipiga Real Madrid Marcelo

Mashabiki wa Sao Paulo wakishangilia timu yao ikiwa ni mtanange wa mwisho kabla awajaanza kuishangilia kwa sana kabla ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia wiki ijayo kwenye Mashndano ya Fifa Kombe la Dunia Nchini Humo Brazil.

Umati Mkubwa wa Mashabiki wa Timu ya Brazil ambapo mashindano ya Kombe la Dunia yatafanyikia wakiwa tayari Uwanjani kwa wingi kuona Timu hiyo mjini Sao Paulo

Serbia wakitoa ujumbe wa....wakitaka kusaidiwa kwa vyovyote vile Nchini mwao Kabla ya mtanange kuanza.
VIKOSI:
Brazil:
Julio Cesar, Dani Alves (Maicon 71), Luiz, Thiago Silva, Marcelo (Maxwell 74), Gustavo, Paulinho (Fernandinho 64), Oscar (Willian 46), Hulk, Fred (Jo 75), Neymar.
Subs Not Used: Jefferson, Dante, Henrique, Ramires, Hernanes, Bernard, Victor.

Serbia: Stojkovic (Lukac 88), Basta (Tomovic 86), Ivanovic, Aleksandar Mitrovic, Kolarov, Dusko Tosic, Matic, Jojic, Tadic (Zoran Tosic 69), Petrovic (Mrdja 86), Markovic (Gudelj 81).
Subs Not Used: Pejcinovic, Djuricic, Stefan Mitrovic, Ljajic, Bisevac, Vulicevic, Lazovic, Brkic.
Ref: Enrique Caceres

No comments:

Post a Comment