Monday, July 14, 2014

KOMBE LA DUNIA: BUTI YA DHAHABU- JAMES RODRIGUEZ! MESSI MPIRA WA DHAHABU, NEUER-GLOVU YA DHAHABU, POGBA-KIJANA BORA!

MARA baada kumalizika Fainali ya Kombe la Dunia huko Maracana, Rio de Janeiro Nchini Brazil ambayo Germany waliifunga Argentina Bao 1-0 na kutwaa Kombe la Dunia, FIFA ilitangaza Tuzo za Wachezaji Bora na Straika wa Colombia, James Rodriguez kutwaa Buti ya Dhahabu.
Rodriguez, ambae Timu yake Colombia ilitolewa kwenye Robo Fainali na Brazil, alipachika Bao 6 kwenye Fainali hizo akifuatiwa na Thomas Muller wa Germany aliekuwa na Bao 5.
Lionel Messi alipewa Mpira wa Dhahabu kwa kuteuliwa kuwa Mchezaji Bora.
Head coach Alejandro Sabella of Argentina looks on with his team after being defeated by Germany 1-0
Nae Kipa wa Germany, Manuel Neuer, ameteuliwa Kipa Bora na kushinda Glovu ya Dhahabu.
Kwa upande wa Vijana, Mchezaji Bora ni Paul Pogba ndie alietwaa Tuzo ya Mchezaji Kijana.
Manuel Neuer of Germany holds the Golden Glove trophy as Lionel Messi of Argentina holds the Golden Ball trophy Manuel Neuer na Lionel MessiGermany celebrate with the World Cup trophy after defeating Argentina 1-0 in extra time
WAGOMBEA
MPIRA WA DHAHABU

Argentina
-Angel Di Maria
-Javier Mascherano
-Lionel Messi


Germany
-Mats Hummels
-Toni Kroos
-Phillip Lahm
-Thomas Muller


Wengine
-James Rodriguez [Colombia]
-Neymar [Brazil]
-Arjen Robben [Netherlands]

GLOVU YA DHAHABU
- Keylor Navas [Costa Rica]
-Manuel Neuer [Germany]
-Sergio Romero[Argentina]


RUZO MCHEZAJI BORA KIJANA
- Memphis Depay [Netherlands]
-Paul Pogba [France]
-Raphael Varane [France]

No comments:

Post a Comment