.jpg)
Na Frank Shija.WHVUM
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mukandala Lufufu inayojishughulisha na kazi ya kutafsiri Filamu kwa Lugha ya Kishwahili Bw. Derick Mukandala maarufu kwa jina la Mzee Lufufu (pichani kulia) amekiri kuwa kazi yake anaifanya kienyeji ili hali akifahamu ni makosa.
Kauli hiyo ameitoa leo katika kikao baina yake na Bodi ya Filamu ambapo alieleza kuwa amekuwa akifanya kazi hiyo kwa muda mrefu bila kuzingatia utaratibu huku akijua kuwa ni makosa kwa mtu kutumia kazi ya msanii mwingine bili idhini yake.
“Nikiri tu kwamba nimekuwa nikifanya makosa kwa kutafsiri Filamu bila kuwa na idhini ya wahusika wa filamu hizo” Alisema Lufufu.
Mzee Lufufu aliongeza kuwa amekuwa akifanya kazi hiyo ya kutafsiri Filamu bila vibali akiamini kuwa hakuna ubatili wowote.
.jpg)
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa siyo dhambi kutafsiri Filamu, ila ni lazima anayetaka kufanya kazi hiyo azingatie dheria za nchi na taratibu zinaotakiwa kuzingatiwa.
Fissoo amesema kuwa sheria ya Filamu nchini kifungu namba 17 kinamtaka anayetaka kufanya kazi ya kutafsiri awasilishe muswada wake katika ofisi za Bodi ya Filamu ili uhakikiwa na wataalamu kabla ya kupewa idhini ya kuendelea na kazi hiyo.
Aliongeza kuwa ili kazi ya kutafsiri Filamu ni sharti mhusika kupata idhini ya mwenye Haki Miliki ya filamu husika hivyo ni vyema kuwasiliana na COSOTA ili kufanya utaratibu wa kupata uhalali akitolea mfano wa Filamu ya Nelia iliyotengenezwa nchini Zimbabwe na baadaye ilifanyiwa tafsiri katika lugha ya Kiswahili hapa jijini Dar es Salaam baada ya kufuata taratibu zote.
No comments:
Post a Comment