BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 7, 2015

CRYSTAL PALACE 2 vs 1 MANCHESTER CITY, MABINGWA WATETEZI HOI TENA UGENINI!! UBINGWA SASA WAUACHIE BLUES!

Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England Manchester City Jana walichapwa 2-1 na Crystal Palace huko Selhurst Park na kuvurugiwa kabisa utetezi wa Taji lao.
Kipigo hiki ni cha 4 mfulilizo cha Ugenini na kimewaacha wakiwa Pointi 9 nyuma ya Vinara Chelsea ambao wana Mechi 1 mkononi na pia kubakishwa Nafasi ya wakiwa pia nyuma ya Arsenal na Manchester United.Bao zilizowaua City hapo Jana zilifungwa na Gllenn Murray Dakika ya 34 na Jason Puncheon Dakika ya 48 wakati Bao la City lilifungwa Dakika ya 78 na Yaya Toure.
Ushindi huu umewarusha Crystal Palace hadi Nafasi ya 11.
Mechi inayofuata kwa City ni Jumapili ijayo huko Old Trafford kwenye Dabi ya Manchester dhidi ya Manchester United.Jason Puncheon akishangilia bao lake la pili kwa City kwa kufanya 2-0 kipindi cha pili dakika ya 48. Dakika ya 78 Yaya Touré alianza kurudisha bao kwa kufanya 2-1.Crystal Palace walienda mapumziko wakiongoza kwa bao la Glenn Murray la dakika ya 34 dhidi ya Wageni wao Man City.
2-0 dakika ya 48 mfungaji ni Jason Puncheon kipindi cha piliCity hoi Ugenini....Selhurst Park!!Chupuchupu Crystal Palace wapate bao kipindi cha kwanza...VIKOSI:
Crystal Palace Wanaoanza 11:
Speroni, Ward, Delaney, Dann, Kelly, McArthur, Ledley, Puncheon, Zaha, Bolasie, Murray
Akiba: Hennessey, Hangeland, Souare, Boateng, Sanogo, Gayle, Ameobi
Manchester City Wanaoanza 11: Hart, Sagna, Kompany, Demichelis, Clichy, Navas, Fernandinho, Toure, Silva, Dzeko, Aguero
Akiba: Caballero, Zabaleta, Mangala, Milner, Fernando, Nasri, Lampard

No comments:

Post a Comment