BUKOBA SPORTS

Friday, April 3, 2015

KOCHA ARSENE WENGER NA MCHEZAJI WAKE OLIVIER GIROUD "BORA" MWEZI MARCH, 2015


Olivier Giroud na Meneja  Arsene Wenger wamepewa Tuzo waote wawili huku Giroud akiwa mchezaji bora wa Premier League na Wenger kuwa Kocha Bora wa Mwezi huo wa Tatu.

Straika wa Arsenal Olivier  Giroud amefunga bao tano katika mechi alizocheza mwezi uliopita wa tatu

Hii ni mara ya 14 Wenger, mwenye umri wa miaka 65, kutwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi katika miaka yake 19 ya kuifundisha Arsenal.
Arsenal kwa sasa iko katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu ya England wakati zikiwa zimebaki mechi nane kabla ya ligi hiyo haijafikia mwisho.
Timu hiyo iko pointi saba nyuma ya vinara Chelsea, ambao wana mchezo mmoja mkononi.
The Gunners itawakaribisha Liverpool iliyopo katika nafasi ya tano kwenye uwanja wa Jumamosi.

Arsenal wako nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu  Premier League kutokana na kushinda mechi zao za mwezi wa tatu na wako nyuma ya pointi 7 ya Chelsea.


USHINDI WA ARSENAL KWA MEZI WA TATU.
March 1 Arsenal 2-0 Everton (1 Giroud goal)
March 4 QPR 1-2 Arsenal (1)
March 14 Arsenal 3-0 West Ham (1)
March 21 Newcastle United 1-2 Arsenal (2)

Giroud analingana na Harry Kane kwa mabao kwa kwezi huo wa tatu lakini wanazidiana kitimu....Arsenal wameshinda mechi zote na Spurs wamefungwa mechi mbili za huo mwezi.

No comments:

Post a Comment