BUKOBA SPORTS

Monday, April 6, 2015

YAMOTO BAND WAFUNIKA GEITA PASAKA, WAFANYA MAAJABU YA MWAKA, MAMIA YA WAKAAZI GEITA WAWASHUHUDIA KWA WINGI..KATIKA UKUMBI WA BURUDANI DESIRE PARK.

Na Faustine Ruta, Geita
Waimbaji wanaounda kundi la “Yamoto Band”Aslay, Becka, Bella na Maromboso wakitoa burudani kwa Wakaazi wa Geita leo Usiku kwenye Sikukuu ya PASAKA kwenye Ukumbi wa Burudani wa Desire Pub wakiongozwa na Kiongozi wao Mkubwa Fella na wakazi hao kuonyesha hali ya kuitikia vilivyo kwa kufurika ndani ya Ukumbi wa Desire Park mkoani humo. Kesho Waimbaji hao wanaelekea Bukoba na Watatoa Burudani kwenye Ukumbi wa Lina's Club uliopo Bukoba mjini na Kisha kesho yake tarehe 7 kuelekea Biharamulo.
Wanamuziki wa Kundi la Yamoto Band wakipagawisha mashabiki stejini.
Bendi inayokuja kasi hapa nchini, Yamoto Band" kundi la vijana wenye vipaji vipya usiku wa kuamkia leo imefanya kufuru ndani ya Ukumbi wa Desire hapa Geita na kuteka Vilivyo Mashabiki wao.
Waimbaji wanaounda kundi la “Yamoto Band”Aslay, Becka, Bella na Maromboso wakitoa burudani kwa Wakaazi wa Geita leo Usiku kwenye Sikukuu ya PASAKA.

Shabiki akiburudika kivyake vyake


















Slay(kushoto) akiwajibika Stejini
Wazee wa Kazi wakiwajibika jukwaani



No comments:

Post a Comment