BUKOBA SPORTS

Saturday, July 25, 2015

KAGAME CUP 2015: ADAMA CITY 0 vs 5 AZAM FC, KIPRE TCHETCHE AONESHA MAKALI YAKE! WAKIIBUKA USHINDI WA KISHINDO!

AZAM FC imefuzu kwa asilimia 100 Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kushinda mechi yake ya tatu na ya mwisho ya Kundi C leo Jumamosi dhidi ya Adama City ya Ethiopia, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Azam iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 katika mchezo huo, huku mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Tchetche akifunga mawili na Farid Mussa, Mudathir Yahya na Aggrey Morris wakifunga bao moja kila mmoja.
Dakika 45 za kwanza zilimalizika Azam wakiwa mbele kwa mabao 3-0, Kipre akianza dakika za sita akimalizia krosi ya Ame Ali ‘Zungu’ na dakika ya 18 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Erasto Nyoni.
Nyoni akamtengenezea Mussa kufunga la tatu dakika ya 31 baada ya kutia krosi maridadi ya chini chini iliyounganishwa kwa guu la kushoto na kinda huyo aliyekuwa pembezoni mwa lango la Adama kushoto.
Kipindi cha kwanza, Adama ilimpoteza mchezaji wake, Eshettu Menna aliyetolewa kwa kadi nyekundu na mwamuzi Issa Kagabo wa Rwanda baada ya kumkwatua kwa nyuma Mussa dakika ya 20.

Kipindi cha pili kilipoanza tu, Yahya akaifungia Azam bao la nne akiunganisha kwa kichwa krosi maridadi Ame Ali ‘Zungu’ dakika ya 46.

Na dakika ya 69 Moges Tadese akaoneshwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu, baada ya kuushika kwa makusudi mpira uliopigwa na Yahya na kusababisha penalti pia.

Kipre alikosa bao la wazi mwishoni mwa kipindi cha kwanza baada ya kumpiga tobo kipa wa Adam City, Yacob Fiseha lakini mpira ukatoka nje sentimita chache.
Beki mzoefu wa kimataifa wa Tanzania, Aggrey akaenda kuifungia Azam bao la tano kwa penalti dakika ya 7

Kwa matokeo haya, Azam inamaliza kileleni mwa Kundi C kwa pointi zake tisa ikifuatiwa na KCCA yenye pointi sita ambazo zote zinakwenda Robo Fainali, wakati Adama imemaliza bila pointi na inarejea nyumbani, huku Malakia ya Sudan Kusini iliyomaliza na pointi tatu inaweza kufuzu kama mshindi wa tatu bora.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Abdallah Kheri, Serge Wawa/Said Mourad dk46, Aggrey Morris/Gardiel Miachel, Mudathir Yahya, Hamid Mao, Jean Baptiste Mugiraneza Ame Ali, Kipre Tchetche/Didier Kavumbangu dk60 na Farid Mussa.

Adama City; Yacob Fiseha, Suleman Mohamed, Wendosen Milkesa, Moges Tadese, Eshetu Menna, Biruk Kelbero, Desalegn Debesh/Wendimeneh Zerihum dk40, Erkyi Hun Tesfaye, Temesigen Gitsadik/Biniyam Ayele dk46, Takele Elemayehu na Yonatan Kebede/Henok Gemtesa dk75.
Mchezaji wa Adama City Eshetu Menna ameondolewa kwa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza baada ya kumfanyia mchezaji wa Azam FC rafu mbaya. Katika kipindi hicho cha kwanza Azam Fc walikimaliza wakiwa mbele ya bao 3-0 dhidi ya Adama City.
Bao za Azam Kipre Tchetche bao mbili na moja ni Mussa.
Kipindi cha pili mapema Mudathir Yahya aliipatia bao la kichwa na kufanya bao kuwa 4-0 dhidi ya Adama City.
Agrey Moris aliifungia bao la tano Azam Fc kwa mkwaju wa penati na Mchezaji wa Adama Fc kuondolewa kwa kadi nyekundu tena baada ya kufanya majanga kwenye eneo hatari na mtanange kumalizika kwa bao hizo 5-0 dhidi ya Adama Fc.


Kesho jumapili kuna michezo miwili ya kumalizia hatua ya kukamisha makundi ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup 2015).
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku macho na masikio ya wapenzi wa soka yakiwa katika mchezo kati ya Yanga SC dhidi ya Kahrtoum ya Sudan. Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 10 kamili jioni.
Kwenye Mechi nyingine ya hii leo mapema KCCA imeifunga bao 1-0 timu ya Malaika, Mtanange uliopigwa kuanzia saa 8 mchana leo jumamosi.
Hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Kagame itachezwa Jumanne, Julai 28 na Jumatano Julai 29 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.









No comments:

Post a Comment