Nchini Afrika Kusini, mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius ataachiliwa huru wiki ijayo, kufuatia uamzi uliyochukuliwa Alhamisi asubuhi wiki hii na Kamati ya kutoa msamaha kwa wafungwa.
Kamati hiyo imekutana Alhamisi hii ili kutathmini ombi la mwanariadha huyo la kuachiliwa huru kwa masharti. Oscar Pistorius alihukumiwa mwaka uliyopita adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia mpezi wake Reeva Steenkamp, mwezi Februari 2013.Oscar Pistorius ataachiliwa huru Oktoba 20 mwaka huu, baada ya kuzuiliwa jela kwa kipindi cha mwaka mmoja. Vyombo vya sheria vya Afrika Kusini vinamuachilia huru kwa masharti mfungwa anayetimiza moja ya sita ya hukumu aliyopewa.
Kwa mujibu wa Idara ya magereza, Oscar Pistorius atapewa kifungo cha nyumbani hadi mwaka 2019, sawa na mwisho wa adhabu rasmi aliyopewa. Msamaha huo wa haraka unaendana na baadhi ya masharti: atafuatiliwa na mwanasaikolojia na atapaswa kufanya kazi za jamii.
Rufaa yatazamiwa kukatwa mwezi Novemba
Hata hivyo, kuachiliwa kwake kunaweza kuwa kwa muda mfupi. Upande wa mashitaka umetoa ulikata rufaa dhidi ya kifungo chake, ukisema kuwa Pistorius angelipaswa kuhukumiwa kwa kosa la " mauaji " na si kwa kosa la " mauaji bila kukusudia ". Kesi hii ya Rufaa itasikilizwa mapema mwezi Novemba mbele ya Mahakama Kuu ya Rufaa. Kama kweli Mahakama hii itabadili uamuzi, kuna hatari Oscar Pistorius awekwe jela kwa kipindi cha miaka kumi.
Siku ya mwisho ya kusikilizwa kesi ya Oscar Pistorius, ambapo Mwendesha mashataka aliomba kifungo cha miaka 10 dhidi ya mwanariadha huyo mlemavu, Oktoba 17 mwaka 2014.REUTERS/Werner Beukes/Pool

No comments:
Post a Comment