BUKOBA SPORTS

Tuesday, June 7, 2016

COPA AMERICA CENTENARIO: ARGENTINA YADHIHIRISHA UBORA WAO, YAANZA KWA KUWACHAPA MABINGWA WATETEZI CHILE KWA BAO 2-1


Mashindano ya kusaka Nchi Bingwa wa Copa América Centenario yameendelea kwa Argentina, wakicheza bila ya Lionel Messi, kuwanyuka Chile 2-1 na Panama kuifunga Bolivia 2-1.
Panama wameichapa Bolivia 2-1 kwqenye Mechi ya Kundi D iliyochezwa huko Orlando Cirtrus Bowl Mjini Orlando, USA kwa Bao zilizofungwa na Blas Perez katika Dakika za 11 na 87 wakati Bolivia likifungwa Dakika ya 54 na Juan Mattia.

Nao Argentina wakicheza huko Levi’s Stadium huko Santa Clara katika Mechi nyingine ya Kundi D waliwafunga Mabingwa Watetezi wa Copa America Chile Bao 2-0 kwa Bao za Kipindi cha Pili za Angel Di Maria, Dakika ya 51, na Dakika ya 591
Bao la Chile lilifungwa Dakika ya 93 na José Pedro Fuenzalida Gana.
"Mashindano haya Copa América Centenario ni mahsusi kusheherekea Miaka 100 ya Copa America, Mashindano ya Shirikisho la Soka la Nchi za Marekani ya Kusini, CONMEBOL, ambayo yalianzishwa Mwaka 1916."
Hii ni mara ya kwanza kwa michuano hii kuchezwa nje ya Marekani ya Kusini.

Haya yatakuwa ni Mashindano ya 45 kufanyika na kawaida yake hufanyika kila baada ya Miaka Minne lakini safari hii CONMEBOL na CONCACAF, Shirikisho la Soka la Nchi za Marekani ya Kaskazini, Kati na Nchi za Visiwa vya Caribbean, walikubaliana kuandaa Mashindano maalum.
Safari hii michuano hii itakuwa na Nchi 16, badala ya 12 za kawaida, kwa kushirikisha Nchi 10 kutoka CONMEBOL na 6 za CONCACAF.
Kawaida Mshindi wa Copa America huiwakilisha Marekani ya Kusini kwenye Mashindano ya FIFA ya Kombe la Shirikisho lakini Mshindi wa Copa América Centenario hatapewa hilo kwani Mwaka Jana Chile, wakiwa Nyumbani kwao, ndio walitwaa Copa America ya kawaida na wao ndio watashiriki Mashindano ya FIFA ya Kombe la Shirikisho Mwakani, 2017, huko Russia.

No comments:

Post a Comment