BUKOBA SPORTS

Thursday, March 29, 2012



Wakiwa katika maandalizi ya kukubabiliana na mchezo mgumu wa marudiano wa kombe la CAF dhidi Es Setif ya Algeria, klabu ya SIMBA imemtimua kiungo wake wa Kimataifa Patrick Mafisango kutokana na utovu wa nidhamu.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha Mafisango ambaye amekuwa akipewa onyo mara kwa mara na uongozi kutona na tabia yake ya ulevi, alirudia tena kitendo hicho hivi karibuni wakati timu yake ikiwa kambini.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana toka kambi ya Simba iliyopo Bamba Beach, Mafisango baada ya kuwa 'tungi' aliporejea kambini alitoa luigha chafu kwa meneja wa timu hiyo Nicodemus Menard Nyagawa pamoja na kocha mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic kabla ya taarifa kufika kwa uongozi na ndipo mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaj Ismail Aden Rage kuagiza atimuliwe.
Mafisango ni mchezaji mzuri ambaye aliingia nchini baada ya kusajiliwa na Azam FC miaka miwili iliyopita, lakini kutokana na matatizo yake ya nidhamu, Wana Lamba Lamba waliamua kubadilishana na mchezal Humud aende Azam na Mutesa ahamie Simba.
Hata Simba baada ya mzunguko wa kwanza wa ligi ilitaka kumtupia virago mchezaji huyo, lakini ikamsamehe na akarudi uwanjani kwa kishindo akiipigia mabao mfululizo timu hiyo.
Haijulikani sasa kama ndio mwisho wake Simba, au yataisha tena na ataendelea na kazi.
Simba inakabiliwa na mechi ngumu ya marudiano ya Kombe la Shiriksiho Afrika mwishoni mwa wiki dhidi ya ES Setif ya Algeria na Mafisango ni miongoni mwa wachezaji muhimu kwa sasa kikosini.

No comments:

Post a Comment