BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 17, 2012

BAYERN MUNICH VS REAL MADRID USO KWA USO LEO


04/17
Bayern
v.
Real Madrid
-2:45 PM (ET)


04/18
Chelsea
v.
Barcelona
-2:45 PM (ET)


04/24
Barcelona
v.
Chelsea
-2:45 PM (ET)


04/25
Real Madrid
v.
Bayern
-2:45 PM (ET)

Leo Jumanne usiku, Bayern Munich watakuwa wenyeji wa Real Madrid Uwanjani Allianz Arena Mjini Munich, Ujerumani katika Mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya UEFA 
Bayern Munich's Dutch Midfielder Arjen Robben Takes

CHAMPIONZ LIGI.
Nusu Fainali ya pili itachezwa Jumatano Uwanjani Stamford Bridge huko London kati ya wenyeji Chelsea na Mabingwa watetezi FC Barcelona.
 Bayern Munich's French Midfielder Franck Ribery (C) And His                                                     kikosi cha Bayern kikipasha jana
Kwa Bayern Munich huu si wakati muafaka kwao kwa vile wanatoka kwenye matokeo mabaya kwao kwenye Ligi ya Bundesliga kufuatia kuchapwa bao 1-0 na Mabingwa watetezi Borussia Dortmund na kutoka sare 0-0 na Mainz juzi matokeo ambayo yamewaacha wakibakia nafasi ya pili nyuma ya Borussia Dortmund kwa Pointi 8 huku Mechi zikiwa zimebaki 3 tu.
Hata hivyo Bayern, iliyo chini ya Kocha Jupp Heynckes, si Timu ya kubeza na wana Wachezaji hatari kama vile Mario Gomez, Franck Ribery na Arjen Robben ambao wana uwezo mkubwa wa kuleta kashkash kwenye Difensi ya Real Madrid.

Masta wengine wa Bayern Bastian Schweinsteiger, Jerome Boateng na Kipa wa Kimataifa wa Ujerumani Manuel Neuer.
Lakini Bayern watamkosa Kiungo wao mahiri David Alaba ambae yuko kwenye kifungo cha Mechi moja baada ya kula Kadi walipocheza na Marseille kwenye Robo Fainali.
Juu ya yote hayo, Bayern Munich itabidi wagangamale maana tishio kubwa toka Real Madrid ni ushambuliaji ambao unaongozwa na Supastaa Cristiano Ronaldo ambae Msimu huu mpaka sasa ameshapachika jumla ya mabao 53 katika Mashindano yote.
Jumamosi iliyopita, Real Madrid, walio chini ya Kocha machachari Jose Mourinho, waliwachapa Sporting Gijon bao 3-1 na kuifikia ile rekodi ya La Liga ya Klabu kufunga bao nyingi kwa Msimu mmoja kwa kufikia mabao 107, rekodi ambayo pia iliwekwa na Real Madrid Msimu wa Mwaka 1989/90 wakati huo wakiwa chini ya Kocha John Toshack.
Wachezaji wengine tishio wa Real katika mashambulizi ni Karim Benzema Gonzalo Higuain.
Makocha wote wa timu hizi mbili wana uzoefu mkubwa na hatua hii ya mashindano haya. Jupp Heynckes, ambaye alikuwa manager wa Madrid katika msimu wa 1998 ambao ulimaliza ukame wa makombe nje ya Spain kwa Real Madrid - ukame ambao ulidumu kwa miaka 32. Alishinda kombe la Champions league na kulipeleka Bernabau lakini kwa bahati mbaya alifukuzwa baada ya Real kumaliza katika nafasi ya nne, points 11 nyuma ya mabingwa Barcelona. Jose Mourinho na rekodi zake za champions league ni hatari, aliiongoza Porto kuchukua kombe hilo nchini Ujerumani in 2004, kabla ya kuwa na Inter Milan na kuiongoza timu kuitandika Bayern Munich katika fainali ya Champions league katika uwanja wa Bernebeu.

Real Madrid wanapigana vita mbili kubwa sasa hivi, wakiwa viongozi wa ligi ya nyumbani wakipgana vikali na Barcelona, hukuwakiwa ndani ya hatua ya nusu fainali ya Champions league. Kwa upande wa Bayern Munich kufungwa kwao na Dortmund na droo yao dhidi ya Mainz imewafanya wawe na hali ngumu ya kugombania ubingwa wa Bundesiliga. Huku joto la presha ya mchezo huo likizidi kupanda ebu tujaribu kuangalia vita zitakazotea uwanjani kati ya wachezaji wa Bayern na Real @Allianz Arena.


RATIBA:
NUSU FAINALI:
Marudiano:
[Mechi kuaanza Saa 3 Dak 45 Usiku Bongo Taimu]
Jumanne Aprili 24
Barcelona v Chelsea
Jumatano Aprili 25
Real Madrid v Bayern Munich
FAINALI
MECHI Kuchezwa Mei 19 Allianz Arena, Munich, Ujerumani



an


Barcelona

03/28
Marseille
0
-
2
Bayern

04/03
Bayern
2
-
0
Marseille



































































No comments:

Post a Comment