BUKOBA SPORTS

Saturday, April 21, 2012

CUF U- 20: NGORONGORO HEROES VS SUDAN LEO UWANJA WA TAIFA


KIKOSI CHA VIJANA U-20 CHA NGORONGORO HEROES

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya Miaka 20, Ngorongoro Heroes, leo inatinga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza na wenzao wa Sudan Mechi ya kwanza ya Raundi ya Kwanza ya Kombe la Afrika kwa U-20.

Timu hizi zitarudiana huko Sudan kati ya Mei 4, 5 na 6 na Mshindi wa Mechi hizi atasonga Raundi ya 2 kucheza na Nigeria mwishoni mwa Mwezi Julai.

Fainali za michuano hii zitafanyika Mwakani huko Nchini Algeria na Timu 4 za kwanza za Fainali hizo za Nchini Algeria zitaiwakilisha Afrika kwenye Kombe la Dunia kwa U-20.

Kocha Kim Poulsen anayeinoa Ngorongoro Heroes ameahidi Kikosi chake kufanya vizuri kwenye mechi dhidi ya Sudan.

Akizungumza jana kwenye mkutano na Waandishi wa Habari, Poulsen amesema Timu yake imejiandaa vizuri kwa mechi hiyo na kiu yao ni kushinda.

Nae Kocha wa Sudan, Azhari Osman El Tahir, amesema ingawa haifahamu vizuri Timu ya Tanzania, lakini wamejiandaa kushinda kwani kwa muda mrefu walikuwa hawajashiriki mashindano ya vijana ya kimataifa.

Viingilio kwa Mechi hii itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia Saa 10 kamili jioni vitakuwa Sh. 3,000, Sh. 5,000, Sh. 10,000 na Sh. 15,000.

Sudan iliwasili nchini juzi ikiwa na Kikosi cha Wachezaji 20, Viongozi kumi na Mwandishi wa Habari mmoja.

Waamuzi wa Mechi hii ni Brian Miiro atakayesaidiwa na Mark Ssonko, Lee Patabali na Denis Batte wote kutoka Uganda.

Ejigu Ashenafi wa Ethiopia ndiye atakayekuwa Kamishna.



RATIBA MECHI ZA RAUNDI YA 1 WIKIENDI HII.


Tunisia vs. Libya

Morocco  vs Mauritania

Uganda vs Mozambique

Central Africa vs RD Congo

Chad vs Sierra Leone

Namibia vs Rwanda

Niger vs Liberia

Tanzania vs Sudan

Zimbabwe vs Botswana

No comments:

Post a Comment