BUKOBA SPORTS

Friday, April 6, 2012

DE GEA AMEANZA KUJIFUNZA MIKIKI MIKIKI YA EPL



Kipa kutoka Spain David de Gea alikuwa njiani kuwa kwenye listi ya Makipa ‘bomu’, Massimo Taibi na Mark Bosnich, waliowahi kusajiliwa na Meneja wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, katika utawala wake hapo Old Trafford lakini hivi karibuni Kipa huyo amejirekebisha na kuonekana dhahiri anastahili kuwa Kipa nambari wani wa Mabingwa hao wa England.




David de Gea, Miaka 21, ambae alisajiliwa kwa Pauni Milioni 18 kutoka Atletico Madrid mwanzoni mwa Msimu na kumfanya Kipa wa bei ghali huko England, alishaanza kupoteza namba hapo Man United ambayo ilikuwa imekamatwa na Kipa toka Denmark Anders Lindegaard baada ya De Gea kufanya makosa yaliyowapa ushindi Blackburn Mwezi Desemba.
Lakini Lindergaard aliumia enka Mwezi Januari na De Gea akarudi kilingeni na kuwa Kipa mpya kabisa.



Akizungumzia hilo, Ferguson amesema: ‘Sasa ametulia. Hakuruhusu makosa yake yamchanganye na sasa anacheza kwa kujiamini. Eneo pekee alilokuwa akilaumiwa ni mipira ya juu. Amesimama imara na alijua nini changamoto. Sasa ameshaanza kuzoea Soka la Uingereza!’

No comments:

Post a Comment