BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 4, 2012

ETO'O AFUTA KESI YAKE NA BARCELONA

Mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon Samuel Eto'o, amefuta kesi dhidi ya klabu ya Barcelona inayohusu malipo yaliyotokana na uhamisho wake wa kwenda Inter Milan.

 
Samuel Eto'o afuta kesi na Barcelona
Samuel Eto'o amekuwa akidai kiasi cha euro milioni tatu sawa na dola milioni 3.99 kutokana na makubaliano ya mwaka 2009.
"Barcelona ingependa kuutangazia ulimwengu kwamba wanamshukuru Samuel Eto'o kwa kuonesha hiari ya kulimaliza shauri hilo," klabu hiyo ilieleza.
"Alikuwa mmoja wa wafungaji hodari wa mabao katika historia ya klabu."
Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Cameroon, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Urusi ya Ligi Kuu ya Anzhi Makhachkala, alihamia Inter kwa makubaliano ya kubadilishana na Zlatan Ibrahimovic.
Ibrahimovic mchezaji wa kimataifa wa Sweden, kwa sasa yupo AC Milan, aliigharimu Barca ada ya euro milioni 46 sawa na dola milioni 61.19, wakati Eto'o thamani yake ilikuwa euro milioni 20 sawa na dola milioni 26.60.

Eto'o madai yake yalikuwa chini ya taratibu za Chama cha Wacheza Kandanda cha Hispania(AFE), ambapo mchezaji ana haki ya kudai asilimia 15 ya mapato ya ada yoyote ya uhamisho.
Kitengo cha sheria cha Barca kilijitetea kwa kudai taratibu za AFE zinafanya kazi kwa uhamisho baina ya vilabu vya Hispania tu.

No comments:

Post a Comment