Drogba akifanya mambo yake jana dthidi ya Spurs
Jana katika Nusu Fainali ya pili ya Kombe la FA iliyochezwa Uwanja wa Wembley, Chelsea wameinyuka Tottenham bao 5-1 na kutinga Fainali itakayochezwa Mei 5 na watakutana na Liverool ambao jana waliwafunga Everton bao 2-1.
Goli lililoleta utata mpaka bossi wa Tot kulaumu refa wa mchezo wa jana ili kwenye picha
Didier Drogba ndie aliefunga bao la kwanza kwa Chelsea Dakika ya 43 na bao la pili la Chelsea kufungwa na Juan Mata huku likigubikwa na utata mkubwa kwamba mpira haukuvuka mstari na pia John Terry alicheza faulo kwa kuwarukia Wachezaji wawili wa Tottenham pamoja na Kipa wao na kuwaangusha wote chini wakati mpira unapigwa golini.
Muda mfupi baadae Tottenham wakafunga bao lao kupitia Gareth Bale lakini kama hilo goli lisingefungwa basi Refa Martin Atkinson angewajibika kumpa Kadi Nyekundu Kipa wa Chelsea Petr Cech kwa kuwangusha Adebayor wakati akienda kufunga na pia kutoa penati.
Ramires alifunga bao la 3, Lampard bao la 4 na Malouda bao la 5.
VIKOSI
Tottenham: Cudicini, Walker, Gallas, King, Assou-Ekotto, Lennon, Modric, Parker, Bale, Adebayor, Van der Vaart
Akiba: Friedel, Giovani, Defoe, Rose, Livermore, Sandro, Nelsen.
Chelsea: Cech, Bosingwa, Terry, Luiz, Cole, Ramires, Lampard, Mikel, Kalou, Drogba, Mata
Akiba: Turnbull, Essien, Torres, Malouda, Meireles, Sturridge, Cahill.
Refa: Martin Atkinson
RATIBA:
FAINALI
UWANJANI WEMBLEY
Jumamosi Mei 5
Liverpool v Chelsea
No comments:
Post a Comment