BUKOBA SPORTS

Friday, April 6, 2012

KASEJA ALIA NA HILA ZA WAARABU

Kaseja

Juma Kaseja, amesema vitimbi wanavyofanyiwa na wenyeji havitawafanya wapunguze ari ya kushinda pambano lao dhidi ya Setif kesho. Akizungumza na tovuti ya Simba, Kaseja alisema wametazama kwa makini matukio mbalimbali yanayofanywa na wenyeji wao na wamebaini yako mambo ambayo lengo lake ni kuwaondoa mchezoni.
“Hebu fikiria, watu wanataka kutusafisha kwa basi kwa masaa sita wakati wanajua kanuni ni masaa mawili tu. Halafu, badala ya kutusafirisha hadi mji wa Setif tulipocheza, wao wametupeleka kwanza mji mwingine na halafu wakatusafirisha kwa basi kuja Setif. Hizi ni mbinu zao lakini tunazijua,” alisema.
Kaseja alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Simba walioitoa Zamalek ya Misri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika miaka kumi iliyopita na anasema hakuna cha ajabu iwapo timu yake itaitoa Setif.
“Katika uzoefu wangu wa soka, timu pekee ya kiarabu ambayo ilitutendea vema ilikuwa ni Harass Al Hadoud ya Misri miaka miwili iliyopita. Lakini hawa walikuwa wema kwa sababu walikuwa wametufunga katika mechi ya kwanza na hivyo hawakuwa na wasiwasi.
“Ukiona Waarabu wanakufanyia vitimbi ujue wana wasiwasi na wewe. Kama hawana hofu, watakupa kila unachohitaji. Nashukuru kwamba tuna wachezaji wazoefu wa kutosha wanaoweza kupambana na lolote,” alisema.

No comments:

Post a Comment