BUKOBA SPORTS

Wednesday, April 4, 2012

KOCHA WA ES SETIF - SIMBA WASUBIRI KICHAPO CHA HATARI.


Kocha wa ES Setif, Alain Geiger ametambia kurejea uwanjani kwa wachezaji wake watatu ambao walikosekana wakati timu hiyo ilipofungwa mabao 2-0 na Simba Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Simba iliifunga ES Setif katika mchezo wa kwanza raundi ya kwanza Machi 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
 

Wachezaji hao ni Abdelmoumen Djabou, Bengoreine Gourmi na Delhoum, ambao pia aliwatumia kwenye mchezo baada ya kuifunga CRB Ain Oussera kwa mabao 3-1, kwenye robo fainali ya mchezo wa Kombe la Algeria na kutinga nusu fainali mwishoni mwa wiki.

Kulingana na taarifa za kwenye mtandao, Setif ilitawala mchezo huo hasa katika kipindi cha kwanza, huku mabao yake yakiwekwa kimiani na Abdelmoumen Djabou aliyefunga dakika ya 13 na 61 na la tatu likifungwa na Delhoum dakika ya 87.

Geiger alisema kurejea kwa Djabou, Gourmi na Delhoum ni faraja kwa kikosi chake katika kuikabili Simba kwani kulikuwa na udhaifu mkubwa mchezo wa kwanza.

“Naamini sasa timu yangu imekamilika, mchezo utakuwa mzuri na tutawapa furaja mashabiki
wetu, ” alisema kocha huyo.

Timu hizo zitarudiana Ijumaa wiki hii mjini Setif, ambapo Simba iliondoka Dar es Salaam juzi na kulala, Cairo Misri, ambapo jana iliondoka kuelekea Algeria.

Wachezaji wa Simba waliopo kwenye msafara ni Juma Kaseja, Ally Mustafa, Nassor Masoud,
Shomari Kapombe, Amir Maftaha, Juma Nyoso, Kelvin Yondani, Victor Costa, Obadia Mungusa, Jonas Mkude, Patrick Mafisango, Mwinyi Kazimoto, Haruna Moshi, Salum Machaku, Uhuru Selemani, Felix Sunzu, Emmanuel Okwi, Edward Christopher, Derick Walulya na Gervais Kago.

Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic alitamba kabla ya kuondoka kuwa wanaenda kupambana na kuhakikisha wanarudi na ushindi.

Simba inahitaji au sare ama isifungwe zaidi ya mabao 2-0 itakuwa imefuzu fainali hizo.
 

No comments:

Post a Comment