Bao mbili za Papiss Cisse zimewapa ushindi Newcastle wa bao 2-0 dhidi ya Liverpool kwenye mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa leo Sports Direct Arena na na kuwafanya wawe na Pointi 53 sawa na Chelsea lakini Newcastle wako nyuma yao na wapo nafasi ya 6 kwa kuwa na tofauti ya mabao hafifu.
Kipigo hiki kimewafanya Liverpool wawe wamepoteza mechi za Ligi 6 kati ya 7 walizocheza mwisho na wapo nafasi ya 8 Pointi moja nyuma ya Mahasimu wao Everton walio nafasi ya 7.
Papiss Cisse alipiga bao la kwanza kwa kichwa kufuatia krosi ya Hatem Ben Arfa katika Dakika ya 19 na Papiss Cisse alifunga bao la pili Dakika ya 59 toka pasi ya Demba Ba [Pichani].
Reina alipompiga kichwa mchezaji na kulimwa red faster.
Mshahara huu hapa kula nyukundu.....
Liverpool walimaliza mechi hii wakiwa Mtu 10 baada ya Kipa wao Pepe Reina kupewa Kadi Nyekundu na Refa Martin Atkinson kufuatia kulipiza kwake baada ya kuchezewa faulo na John Perch.
VIKOSI
Newcastle [4-3-3]: Krul, Simpson, Williamson, Perch, Gutierrez, Guthrie, Tiote, Cabaye, Ben Arfa, Cisse, Ba.
Akiba: Elliot, Ferguson, Santon, Gosling, R.Taylor, Vuckic, Ameobi
Liverpool: Reina, Flanagan, Carragher, Skrtel, Enrique, Gerrard, Spearing, Shelvey, Bellamy, Carroll, Suarez
Akiba: Doni, Aurelio, Maxi, Henderson, Coates, Kuyt, Downing
Refa: Martin Atkinson
No comments:
Post a Comment