BUKOBA SPORTS

Thursday, April 5, 2012

MAMBO MUHIMU KUJUA KABLA YA MCHEZO WA SIMBA NA WAALGERIA JUMAPILI

    Okwi, Machaku na Sunzu wakipasha jioni ya jana huko Algeria.


Wiki hii jumapili, Simba SC ya Dar es Salaam itashuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na ESS Setif ya Algeria katika Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho Afrika, huo ukiwa ni mchezo wa kwanza kabla ya timu hizo kurudiana wiki mbili baadaye mjini Algiers.
Setif inakuwa timu ya tatu kihistoria kumenyana na Simba SC, baada ya awali Wekundu hao wa Msimbazi kutolewa na JET katika Klabu Bingwa Afrika, kabla ba wao kuitoa Al harrach katika Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kwa ujumla Simba ni mabalozi wazuri wa Tanzania katika michuano ya Afrika na wamekuwa wakifanya vema kila wanapomenyana na timu kutoka Kaskazini mwa Afrika.
Kuelelea mchezo huo, bongostaz inakuletea rekodi ya Simba na timu za kaskazini mwa Afrika, zikiwemo za kutoka Algeria. Endelea.

  
LIGI YA MABINGWA AFRIKA:
MWAKA 1974:
NUSU FAINALI:
Simba Vs Mehallal 1-0:   0-1
(Mehalla ilishinda kwa penalti 3-0, ingawa kuna habari za kipa wa Simba, Athumani Mambosasa (sasa marehemu) kufanyiwa fujo, wakati wa upigwaji wa penalti.

MWAKA 1981:
RAUNDI YA PILI:
Simba ilitolewa na JET ya Algeria.
MWAKA 2003:
RAUNDI YA PILI:
Simba (Dsm) Vs Zamalek 1-0
Zamalek (Misri) Vs Simba 1-0
(Simba ilifuzu kwa penaliti 3-2)
MECHI ZA KUNDI A:
Sept. 7/2003:      Simba Vs Ismaili  0-0
Sept. 19/2003:    Ismaili (Msri) Vs Simba 2-1
KOMBE LA WASHINDI
MWAKA 1985
RAUNDI YA PILI
Simba SC Vs Al Ahly (Misri) 2-1 0-2
MWAKA 1996
RAUNDI YA PILI
Simba Vs Al Mokaoulun (Misri) 3-1 0-2 3-3 (Al Mokaoulun walifuzu kwa faida ya bao la ugenini)
MWAKA 2001
RAUNDI YA PILI
Ismailia (Misri) Vs Simba SC 2-0, 0-1, 2-1
(Mechi ya marudiano ilichezwa mara mbili, baada ya mechi ya kwanza kuvunjika dakika ya 46, SImba ikiwa inaongoza mabao 2-0, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam(sasa Uhuru). Ismailia walilalamikia hali ya Uwanja kujaa maji kwamba kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku hiyo, hivyo kugoma kucheza katika mazingira yale na mchezo ukasogezwa mbele kwa siku moja na ndipo wenyeji waliposhinda 1-0. Hivyo Simba kwa kufungwa 2-0 awali mjini Cairo, walijikuta wakitolewa kwa matokeo ya jumla ya kufungwa 2-1.
Mchezo wa kwanza ulitawaliwa na vurugu, Polisi walivamia uwanjani kuwatawanya wachezaji wa Ismailia kwa mabomu ya machozi, waliokuwa wakimzonga refa kwa madai mashabiki wa Simba walimpiga na chupa mchezaji mwenzao mmoja, Emad El-Nahhas.

KOMBE LA CAF/SHIRIKISHO:
MWAK 1993
ROBO FAINALI:
Simba Vs USM El Harrach (Algeria) 3-0 0-2 3-2
MWAKA 2010:
RAUNDI YA PILI:
Aprili 25: Simba Vs Haras El Hodoud 2-1
Mei 8:     Haras El Hodood Vs Simba SC  5 - 1

No comments:

Post a Comment