BUKOBA SPORTS

Tuesday, April 3, 2012

MASTAA TOKA AFRICA WALIONG'ARA ULAYA WIKIENDI


• Cisse, Adebayor waongoza kupiga bao!!



Papiss Demba Cisse na Emmanuel Adebayor wote walipiga bao mbili kila mmoja kwenye Klabu zao katika mechi za Ligi Kuu Englandzilizochezwa Wikiendi hii iliyopita.

Cisse, Straika kutoka Senegal aliesainiwa na Newcastle Mwezi Januari kutoka Freiburg ya Ujerumani, alifunga bao zote mbili pale Newcastle ilipowachapa Liverpool bao 2-0 na sasa amefikisha bao 7 katika Mechi 7 alizochezea Newcastle hadi sasa.

Adebayor, Straika kutoka Togo ambae yuko kwa mkopo Tottenham akitokea Manchester City, alifunga bao mbili Tottenham ilipoipiga Swansea City bao 3-1 huo ukiwa ushindi wa kwanza kwa Tottenham katika mechi 6 za Ligi walizocheza mwisho.




IFUATAYO NI TAARIFA KAMILI KUHUSU WACHEZAJI GANI WA AFRIKA WALIONG’ARA LIGI ZA ULAYA:


ENGLAND

 PAPISS DEMBA CISSE (Newcastle)
Ameanza vizuri na Timu yake mpya Newcastle na kupiga bao 7 katika mechi 7 na Wikiendi hii iliyopita alifunga bao zote mbili za Newcastle ilipoicharaza Liverpool 2-0.
 
EMMANUEL ADEBAYOR (Tottenham)
Kwa sasa, bila shaka, Roberto Mancini anajuta kwa nini alimtoa kwa mkopo!
Bao zake mbili zimewasaidia Tottenham iwafunge Swansea City bao 3-1 na huo ni ushindi wao wa kwanza katika mechi 6 za Ligi ambao umewafanya waifikie kwa Pointi Arsenal walio nafasi ya 3 na pia kujiwekea pengo la Pointi 5 na Timu inayowafuata, Chelsea, walio nafasi ya 5.

VICTOR ANICHEBE (Everton)
Siku zote Meneja wa Everton David Moyes amekuwa akimsifia Straika huyu kutoka Nigeria na Wikiendi alipachika bao la pili lililowapa Everton ushindi wa bao 2-0 dhidi ya West Bromwich Albion.
 
SAMBA DIAKITE (QPR)
Huyu ni Kiungo kutoka Mali ambae yuko kwa mkopo QPR kutoka Nancy ya Ufaransa na alifunga bao lake la kwanza kwa QPR ambalo lilikuwa ni bao la pili na la ushindi kwa QPR walipoipiga Arsenal 2-1.
 
FRANCE
BAKAYE TRAORE (Nancy)
Huyu ni Kiungo kutoka Mali na alifunga bao la kwanza lililowapa Nancy ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Paris Saint-Germain Timu ambayo inapewa nafasi kubwa huko Ufaransa.
 
MAX GRADEL (Saint-Etienne)
Gradel anatoka Ivory Coast alifunga bao la kwanza kwa Timu yake Saint-Etienne lakini ilichapwa 3-2 na Nice.
 
DENNIS OLIECH & KAMEL CHAFNI (Auxerre)
Dennis Oliech wa Kenya na Kamel Chafni wa Morocco walipiga bao zilizowapa Auxerre ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Valenciennes.
Bao la Oliech ni la 10 kwake katika Ligi. 

GERMANY
NANDO RAFAEL (Augsburg)
Straika huyu toka Angola alipiga bao la pili ambalo liliwapa Augsburg ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Cologne.
 
ERIC CHOUPO-MOTING (Mainz)
Eric, kutoka Cameroon, alipiga bao mbili na kuwapa Mainz ushindi wa bao 3-0 walipoifunga Werder Bremen.
 
DIDIER YA KONAN & MAME BIRAM DIOUF (Hanover 96)
Straika kutoka Ivory Coast Ya Konan na yule wa Senegal Mame GiramDiouf, alietokea Manchester United, walipiga bao zilizowapa Hannover ushindi wa 2-1 ju ya Borussia Moenchengladbach.  
 
ITALY
McDONALD MARIGA (Parma)
Parma waliwafunga Lazio bao 3-1 na Mariga kutoka Kenya alifunga bao la kwanza.
 
 

No comments:

Post a Comment