WACHEZAJI WA CHELSEA WAKIPEANA NENO JANA
Straika wa Chelsea Didier Drogba, ambae ndie alifunga bao la ushindi katika Mechi ya kwanza, amesafiri na Timu ya Chelsea kwenda Jijini Barcelona kurudiana na FC Barcelona katika Mechi ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI itayochezwa Jumanne Saa 3 Dakika 45 Usiku Uwanjani Nou Camp.
Drogba, Miaka 34, aliikosa Mechi ya Chelsea ya Ligi Kuu England walipocheza na Arsenal juzi Jumamosi Uwanja wa Emirates na kutoka sare 0-0 baada ya kuwa na maumivu ya goti.
KIPA WA CHELSEA AKIFANYA MAZOEZI MAKALI JANA KWENYE KIWANJA CHA BARCA
CHELSEA KULAMBA £10 MILLIONI WAKIWATOA BARCA NA KUCHUKUA UBINGWA WA ULAYA.
Wachezaji wa Chelsea wamehaidiwa na bosi wao Roman Abramovich kupata bonasi ya £10 million ikiwa watafanikiwa kuifunga Barca, kisha kwenda fainali na kuchukua ubingwa wa kwanza wa ligi ya mabingwa wa ulaya katika historia ya timu hiyo.According to gazeti la The Sun la Uingereza ikiwa Chelsea watafanikiwa kuchukua kombe hilo watapewa kiasi hicho cha fedha huku manager wao wa muda Roberto Di Matteo nae hatoondoka mikono mitupu.
Kila mchezaji wa kikosi cha wachezaji 25 atapokea kiasi cha £350,000 ikiwa watafanikiwa kubeba kombe la ulaya pale Allianz Arena mwezi ujao.
Roberto Di Matteo ambayo bado hajapokea ongezeko la mshahara ukiachana na 1.2millionaliyokuwa akilipwa kwa mwaka kama kocha namba 2 nyuma ya Villas Boas.
Bonasi yake itajadiliwa katika kikao cha baina yake na mmiliki wa The Blues.
Hata hivyo taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema kiungo huyo wa zamani wa klabu atavuta mkwanja unaofikiwa paundi 500,000 kama shukrani kwa kugeuza msimu wa Chelsea - japokuwa bado hajapewa uhakika wa kupewa kazi ya moja kwa moja kama kocha mkuu.
Di Matteo amefungwa mechi moja tu tangu amrithi Villas Boas huku akiwa aemcheza mechi 14.
VIKOSI VITAKAVYOCHEZA LEO.
Chelsea: Petr Cech, Branislav Ivanovic, Gary Cahill, John Terry, Ashley Cole, Frank Lampard, John Mikel Obi, Raul Meireles, Juan Mata, Didier Drogba, Ramires
Akiba: Ross Turnbull, Jose Bosingwa, Michael Essien, Florent Malouda, Salomon Kalou, Daniel Sturridge, Fernando Torres.
Barcelona: Valdes; Alves, Puyol, Mascherano, Adriano; Xavi, Busquets, Iniesta; Sanchez, Messi, Fabregas.
Akiba: Pinto, Pique, Thiago, Kieta, Barta, Cuenca, Pedro.
No comments:
Post a Comment