BUKOBA SPORTS

Wednesday, May 23, 2012

COPA DEL REY: ATHLETIC BILBAO V BARCELONA IJUMAA MEI 25 SAA 5:00 USIKU.

FC Barcelona, baada ya kupokonywa Ubingwa wa Spain na  Mahasimu wao Real Madrid na ule Ubingwa wao wa Ulaya uliochukuliwa na Chelsea, Ijumaa Usiku wanaingia Uwanjani kusaka Taji lao la 26 la Copa del Rey watakapokutana na Athletic Bilbao ambao nao mapema Mwezi huu walilikosa Taji la EUROPA LIGI walipochapwa bao 3-0 na Atletico Madrid.
Msimu huu Athletic Bilbao na FC Barcelona zimekutana mara mbili kwenye La Liga na katika Mechi ya kwanza iliyochezwa San Mames Timu hizi zilitoka sare ya bao 2-2 na Barca ndio walisalimika kipigo baada ya Lionel Messi kusawazisha Dakika ya mwisho.
 
Katika Mechi ya marudiano iliyochezwa Nou Camp Barca walishinda bao 2-0 lakini kwenye Mechi hiyo Bilbao walicheza bila ya Mastraika wao watatu Iker Muniain, Ander Herrera na Fernando Llorente lakini itakuwa maajabu makubwa kama Kocha Bilbao Marcelo Bielsa atawaacha tena Mastraika hao.

Athletic Bilbao - Wachezaji wa kuchunga
Bila shaka Fernando Llorente ndie hatari kwani Msimu huu amefunga bao 17 katika Mechi 32 za Ligi alizoichezea Bilbao.
Vilevile, Bilbao wanao Markel Susaeta na Iker Muniain ambao pia ni wakali na wanaweza kuisumbua ngome ya Barca.
 
Ingawa takwimu za Muniain si za kutisha kwa Msimu huu lakini Susaeta amepachika bao 6 na kutoa pasi za magoli 7 Msimu huu.
Kwenye Kiungo, Abder Herrera ndio mashine ya Bilbao.

FC Barcelona - Wachezaji wa kuchunga
Bila kusema, siku zote Lionel Messi ndio Mtu hatari kwa Barca.
Lakini mbali ya Messi, wapo Iniesta, Xavi na Pedro ambao ni tishio kubwa kwa Timu yeyote Duniani na, bila shaka, watataka kumuaga Kocha wao Pep Guardiola katika Mechi yake ya mwisho kwa ushindi mnono.
 Messi / PHOTO: Miguel Ruiz - FCB

No comments:

Post a Comment