Wakala wa Kiungo wa Ubelgiji Eden Hazard ametamka kuwa wao wamepokea ofa zinazokubalika kutoka kwa Manchester City, Manchester United na Chelsea na sasa kilichobaki ni kwa Mchezaji huyo kuamua tu kukubali ofa ya Klabu ipi.
Wakala huyo, John Bico, amesema: ‘Hatuko tena kwenye majadiliano, tumeshakubaliana na Klabu zote! Hamna kukubali ofa ya juu! Eden amesema anataka kuamua kabla ya Juni 2 baada ya Ubelgiji kucheza na Montenegro na England kisha aende vakesheni.’
Lakini dalili zinaonyesha Chelsea ndio wanaweza kumpata Mchezaji huyo kwa sababu wao wako tayari kumlipa Mchezaji huyo mwenye umri wa Miaka 21 Mshahara wa Pauni 200,000 kwa Wiki huku Klabu za Manchester, Man City na Man United, zikiwa haziko tayari kumlipa zaidi ya Pauni 110,000 kwa Wiki na pia kutoa dau la uhamisho la karibu Pauni Milioni 35 ambazo Klabu yake ya Ufaransa Lille inasemekana inataka baada ya kuona ushindani mkubwa wa kumnunua.
NUKUU YAKE!
"Of course it makes you think as Chelsea have won the Champions League. They're a big team and will be playing in the Champions League next season. They have great players and I always said I wanted to be playing. I think there is the possibility to play as well.
"I still don't know [which club I will join] yet, otherwise I would have announced it today. Nothing is done yet but it will happen soon."
No comments:
Post a Comment