Straika kutoka Ivory Coast Didier Drogba amewaambia Wachezaji wenzake kuwa hapendi kuwekwa benchi hivyo ataondoka Chelsea.
Habari hizi zometolewa katika Gazeti la Ufaransa, France Football, na zinadai Drogba, Miaka 34, alitokwa na machozi alipowaambia Wachezaji wenzake juu ya Basi la ghorofa lililokuwa likiwatembeza Mitaa ya London wakisheherekea Ubingwa wao wa Ulaya Siku ya Jumapili.
Drogba ndiye aliyefunga bao la Chelsea kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Jumamosi iliyopita na pia kufunga penati ya mwisho Chelsea walipowabwaga Bayern Munich kwa penati 4-3 baada ya kutoka sare ya bao 1-1.
Inadaiwa Drogba alisema: ‘Hatutakuwa pamoja Msimu ujao. Nimeamua kuondoka!’
Mkataba wa Drogba na Chelsea, Timu aliyojiunga nayo Mwaka 2004 akitokea Marseille ya Ufaransa, unamalizika hivi karibuni lakini kuna tetesi Chelsea inataka kumwongezea muda zaidi.
Magazeti ya Uingereza yamekuwa yakimuunganisha Drogba na Klabu ya China, Shanghai Shenhua ambayo Mchezaji mwingine wa zamani wa Chelsea, Nicolas Anelka, ndie Kocha-Mchezaji.
No comments:
Post a Comment