BUKOBA SPORTS

Wednesday, May 9, 2012

EUROPA LIGI FAINALI: BILBAO V ATLETICO MADRID HAPATOSHI LEO

Athletic Bilbao's Fernando Llorente
LEO Jumatano Usiku saa 3.45, Klabu mbili za Spain, Athletic Bilbao na Atletico Madrid, ambazo ziko chini ya Makocha toka Argentina, zitaingia National Arena huko Bucharest, Romania kucheza Fainali ya UEFA EUROPA LIGI.
 Heated: Rivals players clash after the final whistle
Msimu huu Timu hizi zishacheza mara mbili kwenye La Liga kwa Bilbao kushinda kwao 3-0 na Atletico kujibu mapigo kwa ushindi wa bao 2-1.
 
Atletico wako chini ya Kocha Diego Simeone na Bilbao ipo mikononi mwa Marcelo Bielsa.
Simeone aliwahi kuwa Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Argentina kwa Miaka minne chini ya Kocha wa Timu hiyo wakati huo, Marcelo Bielsa, na wakati huo alimudu kuweka rekodi ya kuichezea Argentina Mechi nyingi, Mechi 106, rekodi ambayo aliiweka kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2002.
Ni Makocha watatu tu waliotoka nje ya Bara la Ulaya ambao wameweza kutwaa Kombe hili na hao wote ni kutoka Argentina, ambao ni Luis Carniglia akiwa na Real Madrid, Helenio Herrera na Inter Milan na Alfredo di Stefano akiwa na Valencia.
Lakini, Diego Simeone anaweza kuwa Mtu wa tatu kutwaa Taji hili akiwa Mchezaji na pia Kochakwani alishawahi kulitwaa alipokuwa akiichezea Inter Milan Mwaka 1998, wakati huo likiitwa UEFA Cup.
Dino Zoff alitwaa Mwaka 1977 akichezea Juventus, walipoifunga Bilbao, na Mwaka 1990 akiwa Kocha.
Huub Stevens alishinda Kombe hili akiwa Mchezaji wa PSV Eindhoven Mwaka 1978 na kama Kocha Mwaka 1997 akiwa na Schalke.
Kwa Wachezaji, Straika wa Atletico Madrid, Falcao, pengine ataweka rekodi ya kuwa Mchezaji pekee kwenye historia ya Mashindano haya kuwa Mfungaji Bora kwa Miaka miwili mfululizo.
Msimu huu, yeye amefunga goli 10 na amefungana juu Nambari wani na Straika wa Schalke Klaas-Huntelaar.
Msimu uliopita, Falcao, anaetoka Colombo, alifunga bao 17 na kuweka rekodi ya ufungaji bora akiwa na FC Porto ambao walitwaa Kombe hili.
Lakini Athletic Bilbao wanae pande la Mtu, Fernando Llorente, ambae nae hayuko nyuma kwa mabao kwani kwenye Mashindano haya Msimu huu ashatingisha kamba mara 7.

FAINALI
Jumatano Mei 9
SAA 3 Dak 45 Usiku
National Arena Bucharest, Romania

No comments:

Post a Comment