Barton kulia akizunguana na Tevez anayeamuliwa na wachezaji wenzake wa Man City
Nahodha wa Queens Park Rangers Joey Barton jana amefungiwa Mechi 12 na kutwangwa Faini ya Pauni 75,000 na Chama cha Soka England, FA, baada ya kupatikana na hatia kwa makosa mawili ya utovu wa nidhamu na kuleta vurugu.Barton, Miaka 29, alimpiga kipepsi Carlos Tevez wa Manchester City kwenye Mechi ya mwisho ya Ligi Kuu England iliyochezwa Uwanja wa Etihad Mei 6 kwenye tukio ambalo mpira haukuwepo kwao na Refa Mike Dean kumpa Kadi Nyekundu.
Akiwa anatoka nje ya Uwanja, Joey Barton akampiga teke Mchezaji mwingine wa Man City, Sergio Aguero na kujaribu kumpiga kichwa Vincent Kompany.
Kwa kosa la Kadi Nyekundu, Joey Barton atatumikia kifungo cha Mechi 3 lakini kwa vile alishawahi kutolewa kwa Kadi Nyekundu Msimu huu adhabu inaongezwa kuwa Mechi 4.
Matukio yaliyowahusu Aguero na Kompany yaliifanya FA kumfungulia mashitaka mawili na kumpa Kifungo cha Mechi 8 baada ya kupatika na hatia na kufanya jumla Mechi ambazo amefungiwa kuwa 12.
MIKASA YAKE:
-2004, akiwa Man City alimwunguza jichoni Mchezaji Chipukizi James Tandy
-2007, alimpiga Mchezaji mwingine Ousmane Dabo hadi akatibiwa Hospitalini
-2008 alifungwa Jela Miezi 6 kwa kushambulia na kujeruhi Mtu.
No comments:
Post a Comment