Mara baada ya Didier Drogba kutangaza na Chelsea kuthibitisha kuondoka kwake mwishoni mwa Juni, Mabingwa hao wa Ulaya wamethibitisha kuwatema José Bosingwa na Salomon Kalou.
Chelsea imekataa kurefusha Mkataba na Bosingwa licha ya kuwepo kipengele cha kufanya hivyo na pia imekataa kumuongeza Mkataba Kalou ambae Mkataba wake unakwisha.
Wachezaji wengine, Florent Malouda, Michael Essien na Paulo Ferreira, wote wakiwa wamebakisha Mwaka mmoja mmoja kwenye Mikataba yao, wanategemewa kufanya mazungumzo na uongozi wa Chelsea kuhusu Mikataba mipya.
Mkongwe Frank Lampard, ambae bado ana Miezi 12 kwenye Mkataba wake, anategemewa kukubali ofa mpya aliyopewa ya kuongezewa Mkataba.
Hadi sasa Chelsea haina Meneja wa kudumu baada ya kutimuliwa Andres Villas-Boas na kuwekwa Roberto Di Matteo kama Meneja wa muda ambae alifanikisha Chelsea kutwaa FA Cup na UEFA CHAMPIONZ LIGI lakini inategemewa Mmiliki wa Klabu Roman Abramovic atakutana hivi karibuni na Bodi ya Klabu kuamua nani awe Meneja wao.
Chelsea tayari imewachukua Chipukizi Marko Marin na Kevin De Bruyne na imeshatoa ofa kuwasajili Kiungo wa Lille Eden Hazard na yule wa Sao Paulo Lucas Moura ingawa bado usajili wao haujakamilika.
Pia, Klabu hiyo ya Stamford Bridge inategemewa kuwarudisha Klabuni Kipa wake Thibaut Courtois, aliekuwa kwa mkopo Atletico Madrid, na Yossi Benayoun aliekuwa Arsenal pia kwa mkopo.
No comments:
Post a Comment