Masaa machache baada ya kutoka Marekani kuzungumza na wamiliki wa klabu ya Liverpool, leo kocha King Kenny Dalglish ametimuliwa kazi ya ukocha pale Anfield.
Kenny Dalglish anaondoka Liverpool miezi 16 baada ya kuichukua timu hiyo baada ya kuondoka kwa kocha Roy Hodgson mwezi January 2011. Dalglish ambaye ameiongoza Liverpool kubeba kombe la Carling Cup msimu huu kabla hawajafungwa na kwenye fainali ya FA Cup dhidi ya Chelsea.
Lakini kushika nafasi ya nane kwenye premier league kulikuwa chini ya mategemeo ya wamiliki waliotumia kiasi kingi cha pesa wakitegemea angalau kupata nafasi ya kushiriki kwenye ligi ya mabingwa ya ulaya.

Klabu ya Liverpool ilikaa kimya kwa muda kuhusu mustakabli wa Kocha Kenny Daglish na majaliwa ya kuendelea kukaa katika klabu hiyo, lakini leo kimya kingi kikawa na mshindo mkuu.
Hapo jana nchini England kulisikika tetesi za kwamba huenda akafanywa kuwa miongoni wa watu katika klabu hiyo lakini kumbe zilikuwa ni tetesi tu.
Hapo jana nchini England kulisikika tetesi za kwamba huenda akafanywa kuwa miongoni wa watu katika klabu hiyo lakini kumbe zilikuwa ni tetesi tu.
Dalglish alipokaribishwa Liverpool na Andy Carroll na Luis Suarez Anfield mwezi Februari 2011
Licha ya kutwaa kikombe cha Carling kwa mikwaju ya Penati dhidi ya Cardiff na kufika fainali ya FA na kunyukwa na Chelsea mabao 2-1.
Dalglish alitumia mamilioni ya fedha kununua wachezaji awa Charlie Adam, Jordan Henderson, Stewart Downing na Alexander Doni .
Daglish na msaidizi wake Steve Clarke walikuwa wamesafiri kuelekea Boston kwa mazungumzo na mmiliki wa Klabu hiyo kama ataendelea kubakia kuwa meneja wa The Reds.
Daglish anashutumiwa sana na wadau wa soka kwa kutumia kiwango cha Paundi milioni 100 kwa ajili ya kununua wachezaji wapya na wameshindwa kuonyesha uwezo licha ya kutaka kuwa miongoni mwa klabu 4 za juu katika msimu huu wa EPL.
No comments:
Post a Comment