BUKOBA SPORTS

Thursday, May 3, 2012

LA LIGA: REAL MADRID WATWAA UBINGWA WAO WA 32 BAADA YA KUICHAPA ATHLETIC BILBAO BAO 3-0

Jana Real Madrid wametwaa Ubingwa wao wa 32 huko Spain, huo ni Ubingwa wa 7 kwa Kocha wao Jose Mourinho katika Nchi 4 tofauti, na kuurudisha tena Santiago Bernabeu baada ya Miaka minne.
 
      LEO REAL MADRID WATACHEREHEKEA CIBELES
Jana Real Madrid walinyakuwa Ubingwa wa La Liga ugenini Uwanja wa Estadio San Mames walipoifunga Athletic Bilbao bao 3-0.
 
Licha ya mapema Ronaldo kukosa penati, mabao ya Gonzalo Higuaín, Mesut Ozil and Ronaldo yaliwapa Ubingwa huo huku wakiwa na Mechi mbili mkononi.
 Party time: Real Madrid celebrate as they win the La Liga title for the first time in four years
 Real Madrid Wakifurahia ushindi wao wa La Liga kwa mara ya kwanza wa miaka minne(4)
Mara baada ya kuchapwa 2-1 na Real Madrid Siku 11 zilizopita, Kocha wa waliokuwa Mabingwa watetezi Barcelona, Pep Guardiola, alikiri Real ndio Mabingwa lakini Jumapili iliyopita Barca iliwachapa Rayo Vallecano bao 7-0 na kuuchelewesha Ubingwa huo kwa Real na jana Barca walicheza mapema na kuichapa Malaga 4-0 na hivyo ilibidi Real Madrid waifunge Athletic Bilbao ili watwae Ubingwa.
 Real Madrid's players celebrate
                 Huu ni Msimu wa Rekodi kwa Real Madrid.
Real, wamefungwa Mechi mbili tu Msimu huu, zile dhidi ya Barca na Levante, na wakishinda Mechi zao mbili zilizobaki watafikisha Pointi 100 na kuivunja rekodi ya Barca ya Pointi 99.
 Real Madrid's players celebrate
Tayari Real wamevunja rekodi ya kufunga bao nyingi kwa Msimu mmoja, rekodi ya bao 107, na sasa wana mabao 115 huku 44 yakifungwa na Cristiano Ronaldo.
 Denied: Gorka Iraizoz saves a penalty from Ronaldo (above) but Gonzalo Higuain opened the scoring (below)
 Gorka Iraizoz akiokoa  penati ya Ronaldo  lakini Gonzalo Higuainakafuta kosa hilo kwa kuichapa goli

Gonzalo Higuain opened the scoring
Ronaldo yuko nyuma ya Lionel Messi ambae jana alipiga hetriki na kufikisha bao 46 kwenye La Liga na ana jumla ya bao 68 Msimu huu na kuivunja rekodi ya Mjerumani Gerd Muller ya kufunga bao nyingi Ulaya katika Msimu mmoja aliyoweka Mwaka 1972/3.
Kwa Jose Mourinho Ubingwa huu ni rekodi maalum kwake.
 Doubling up: Mesut Ozil added a second for Madrid (above) as Mourinho celebrated (below)
Sasa ameshatwaa Ubingwa katika Nchi 4 lakini si yeye pekee aliewahi kufanya hivi kwani Ernst Happel and Giovanni Trapattoni wameshatimiza hayo.
 Real Madrid's coach Jose Mourinho (L) celebrates
                             JOSE MOURINHO JINO NJE NJE!
Happel ameshatwaa Ubingwa akiwa Nchini Holland, Belgium, Germany na Austria na Trapattoni kwenye Nchi za Italy, Germany, Portugal na Austria.
Lakini Kocha kutoka Croatia Tomislav Ivic ameshatwaa Ubingwa Nchini Yugoslav, Holland, Belgium, Greece, Portugal na France.
Ukiacha hayo, Jose Mourinho ametimiza lile lililompeleka Real Madrid na nalo ni kuwabwaga FC Barcelona.

No comments:

Post a Comment