Fabrice Muamba akiwapungia mashabiki mkono jana kwenye uwanja wa Bolton
Fabrice Muamba alirejea Bolton usiku huu na kumwaga machozi mbele ya mashabiki baada ya kipindi kisichopungua wiki sita tangu apatwe matatizo ya moyo uwanjani na kuzimia.
Mchumba wa Muamba (Shauna) pia alikuwepo uwanjani hapo Reebok Stadium jana kushudia pambano
Akionekana mwenye afya tele na bashasha, Muamba alitokwas machozi wakati akisalimia mashabiki kwenye Uwanja wa Reebok.
'natamani ningecheza leo,''alisema Muamba.
'Hii ni sehemu maalum: sapoti imekuwa kubwa na ninafurahia hilo,'' Muamba alisema. ''Niko sawa. Nazidi kuimarika kila siku. nafurahi kurudi, nina furaha kuweza kuzungumza na watu tena na kutembea mwenyewe.
No comments:
Post a Comment