KLABU ya Newcastle United imeisogelea Arsenal katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England hadi kubaki inazidiwa pointi moja tu, kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Chelsea usiku huu. Papiss Cisse alifunga bao la kwanza Uwanja wa Stamford Bridge kwa shuti kali la mguu wa kulia lililojaa nyavuni kipindi cha kwanza.
Bao la pili na la 13 katika mechi 12 tangu ajiunge na timu hiyo Januari, lilikuwa moja ya mabao bora kuwahi kutokea msimu huu - baada ya kuambaa wingi ya kushoto na kuupiga mpira kwa upande wa nje wa kiatu cha na kumtungua kipa Petr Cech.
Kwa Alan Pardew, haikuwa tu kufuta machungu ya kufungwa 4-0 na Wigan Athletic, lakini pia ushindi wake wa kwanza katika Jiji la London tangu awasili Tyneside Desemba mwaka 2010.
Roberto Di Matteo apagawa ... asema alijua kuwa alikuwa na kibarua kigumu...
PAPISS CISSE ALIYEIMALIZA CHELSEA AKISHANGILIADrogba Hoi ashika kiuno !!
No comments:
Post a Comment