BUKOBA SPORTS

Friday, May 11, 2012

MSAIDIZI WA WENGER PAT RICE ATANGAZA KUNG'ATUKA ARSENAL!, KUONDOKA RASMI JUMAPILI

  Thanks for the memories: Pat Rice is quitting as Arsenal assistant manager
BEKI wa zamani Steve Bould kuchukua nafasi!!
 Come in No 2: Steve Bould will be Arsene Wenger's new assistant
 Steve Bould
Pat Rice, Meneja Msaidizi wa Arsenal, ametangaza kustaafu kuitumikia Arsenal na Jumapili ndio itakuwa Siku yake ya mwisho kukaa Benchi la Arsenal watakapokuwa ugenini kucheza Mechi ya mwisho ya Msimu wa  Ligi Kuu England na West Bromwich Albion.
Rice amekuwa Meneja Msaidizi tangu Wenger ajiunge hapo Mwaka 1996.
 Right hand man: Wenger and Rice have worked together since 1996
 Wenger na Rice wamekuwa pamoja tangu  1996
Rice, Miaka 62, alijiunga na Arsenal Mwaka 1964 akiwa Mchezaji wa Timu ya Vijana na Mwaka 1971 alitwaa Mataji mawili, Ligi na FA Cup, na Mwaka 1979 aliiongoza Arsenal kama Nahodha kwenye Fainali ya FA Cup.
Aliichezea Arsenal Mechi 528 kwa Misimu 14.
Akiwa kama Msaidizi wa Wenger, Pat Rice alishinda Mataji 7 makubwa ambayo ni Ubingwa wa Ligi Kuu, mara 3, na FA Cup 4.
Akimuongelea Rice, Wenger alitamka: ‘Pat ni Nguli wa kweli kwa Arsenal. Maisha yake yote yako kwa Arsenal akionyesha uaminifu na mapenzi makubwa!’
Nafasi ya Pat Rice itachukuliwa na Steve Bould, Mchezaji wa zamani wa Arsenal, ambae ni Kocha wa Timu ya Vijana kwa Miaka 11 iliyopita.

No comments:

Post a Comment