BUKOBA SPORTS

Monday, July 2, 2012

AFCON 2013: TIMU 30 ZATENGWA MAKUNDI MAWILI KWA DROO YA MWISHO

  

:-DROO kufanyika Julai 5  

:-RAUNDI ya Mwisho ya Mtoano kuchezwa Septemba na Oktoba

Timu 30 ambazo zitaingia kwenye Droo ya kupanga Mechi 15 za Raundi ya Mwisho ya Mtoano ya AFCON 2013, Kombe la Mataifa ya Afrika, ambayo itafanyika Mjini Johannesburg, Afrika Kusini hapo Julai 5, zimetenganishwa na CAF katika Makundi mawili, moja likiwa KUNDI A na la pili KUNDI B.
Katika Droo hiyo, Timu toka KUNDI A itapangiwa mpinzani kutoka KUNDI B na kuwekwa kwenye KIKUNDI kipi kumezingatia mafanikio ya Nchi husika katika michuano ya AFCON mitatu iliyopita na hivyo zile ambazo zimekuwa na matokeo bora kwenye AFCON zimewekwa KUNDI A.
Raundi ya Mwisho ya Mtoano ndio itakayotoa Nchi 15 zitakazocheza Fainali huko Afrika Kusini pamoja na Wenyeji hao kuanzia Januari 19 hadi Februari 10, Mwakani.
Timu hizo 30 zitakazoingia kwenye Droo ni Timu 14 zilizoshinda Raundi ya Pili ya Mtoano pamoja na Timu 16 zilizocheza Fainali za AFCON 2012 huko Nchini Equatorial Guinea na Gabon mwanzoni mwa Mwaka huu.
Mechi za Raundi ya Mwisho ya Mtoano zitachezwa kwa mtindo wa Nyumbani na Ugenini huku Mechi za kwanza zikichezwa kati ya Septemba 7 hadi 9 na marudiano ni Oktoba 12 hadi 14.
KUNDI  (A)
-Algeria
-Angola
-Burkina Faso
Cameroun
-Ivory Coast
-Gabon
-Ghana
-Guinea
-Equatorial Guinea
-Mali
-Morocco
Nigeria
-Sudan
-Tunisia
-Zambia

KUNDI (B)
-Botswana
-Cape Verde
-Central African Republican
-Ethiopia
-Liberia
-Libya
-Malawi
-Mozambique
-Niger
-Congo DR
-Senegal
-Sierra Leone
-Togo
-Uganda
-Zimbabwe

No comments:

Post a Comment