BUKOBA SPORTS

Monday, July 9, 2012

COPA COCA COLA: ROBO FAINALI KUPIGWA KESHO NA JUMATANO

TFF_LOGORobo Fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 inayokutanisha Vijana wenye umri chini ya Miaka 17 inaanza kesho Julai 10 kwa Timu nne kuumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salam na kumalizika Jumatano kwenye Uwanja huo huo.
RATIBA:
ROBO FAINALI
Jumanne Julai 10
Uwanja wa Karume, Dar es Salaam
Temeke v Mjini Magharibi [Saa 2 na Nusu Asubuhi]
Mara v Morogoro [Saa 10 Jioni]
Jumatano Julai 11
Kinondoni v Mwanza [Saa 2 na Nusu Asubuhi]
Dodoma v Tanga [Saa 10 Jioni]
NUSU FAINALI==Julai 13
Uwanja wa Karume, Dar es Salaam
Temeke/Mjini Magharibi v Kinondoni/Mwanza
Mara/Morogoro v Dodoma/Tanga
FAINALI==Julai 15 [Pamoja na kutafuta Mshindi wa 3]
Uwanja wa Karume, Dar es Salaam
TAARIFA KAMILI YA TFF:
Release No. 112
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Julai 9, 2012
ROBO FAINALI COPA COCA-COLA 2012
Robo Fainali ya michuano ya Copa Coca-Cola 2012 inayokutanisha vijana wenye umri chini ya miaka 17 inaanza kesho (Julai 10 mwaka huu) kwa timu nne kuumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salam.
Temeke na Mjini Magharibi ndizo zitakazocheza robo fainali ya kwanza kuanzia saa 2.30 asubuhi. Mara iliyoivua ubingwa Kigoma itacheza robo fainali ya pili dhidi ya Morogoro kwenye uwanja huo huo.
Robo Fainali ya tatu itachezwa keshokutwa (Julai 11 mwaka huu) kwa kuzikutanisha timu za Kinondoni na Mwanza. Mechi hiyo itaanza saa 2.30 asubuhi na kufuatiwa na nyingine kati ya Dodoma na Tanga itakayoanza 10 kamili jioni.
Nusu fainali ya michuano hiyo iliyoanza Juni 24 mwaka huu katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ikishirikisha timu 28 itafanyika Julai 13 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
Mshindi wa mechi kati ya Temeke na Mjini Magharibi, na Kinondoni dhidi ya Mwanza ndiyo watakaocheza nusu fainali ya kwanza. Nusu fainali ya pili itakuwa mshindi wa mechi ya Mara na Morogoro dhidi ya mshindi wa mechi ya Dodoma na Tanga.
Fainali itafanyika Jumapili (Julai 15 mwaka huu). Mechi zote kuanzia hatua ya robo fainali hadi fainali zitafanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment