BUKOBA SPORTS

Monday, July 9, 2012

FEDERER AONGOZA ORODHA ZA ATP.


Serena Williams(kushoto) na Roger Federer wakipozi pamoja na mataji yao ya Wimbledon.
NYOTA wa mchezo wa tenisi Roger Federer amekamata usukani tena wa wachezaji nyota wa mchezo huo akifikia rekodi ya Pete Sampras ambaye aliweka rekodi ya kuwa namba moja katika orodha za ubora wa mchezo huo duniani kwa muda wa wiki 286. Federer ambaye ana umri wa miaka 30 anaongoza katika orodha hizo ikiwa ni mara yake ya kwanza toka Juni 2010 baada ya kumfunga Andy Murray katika fainali na kunyakuwa taji lake la saba la Wimbledon. Nyota huyo raia wa Switzerland amechukua nafasi ya Novak Djokovic ambaye ameshuka mpaka nafasi ya pili huku Rafael Nadal naye akiporomoka kwa nafasi moja mpaka ya tatu wakati Murray amebaki katika nafasi yake ya nne. Kwa upande wa wanawake Victoria Azarenka ambaye aliishia nusu fainali katika michuano hiyo ameshika usukani kwenye orodha hiyo akichukua nafasi ya Maria Sharapova aliyeporomoka kwa nafasi moja wakati bingwa wa michuano hiyo Serena Williams amepanda mpaka nafasi ya nne kutoka ya sita aliyokuwepo hapo mwanzo. Orodha Kamili ni kama zinavyoonekana hapo chini.
ATP MEN'S RANKINGS. 
1 Roger Federer (Swi) 2 Novak Djokovic (Ser) 3 Rafael Nadal (Spa) 4Andy Murray (GB) 5 David Ferrer (Spa) 6 Jo-Wilfried Tsonga (Fra) 7Tomas Berdych (Cze) 8 Janko Tipsarevic (Serbia) 9 Juan Martin del Potro (Arg) 10 Nicolas Almagro (Spa)

WTA WOMEN'S RANKINGS.
1 Victoria Azarenka (Blr) 2 Agnieszka Radwanska (Pol) 3 Maria Sharapova (Rus) 4 Serena Williams (USA) 5 Samantha Stosur (Aus) 6Petra Kvitova (Cze) 7 Angelique Kerber (Ger) 8 Caroline Wozniacki (Den)9 Sara Errani (Ita) 10 Marion Bartoli (Fra)

No comments:

Post a Comment