BUKOBA SPORTS

Saturday, July 28, 2012

KAGAME CUP: YANGA BINGWA TENA BAADA YA LEO KUIFUNGA AZAM FC GOLI 2-0!



Timu ya YANGA ya Tanzania imefanikiwa kulitwaa tena kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati baada ya kuifunga timu ngeni kwenye mashindano hayo, Azam, kwa 2-0 Jumamosi, mjini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa kimataifa kutoka Uganda Hamis Kiiza alifunga bao la kwanza dakika ya 44 na Said Bahanuzi akaongeza kipindi cha dakika za nyongeza kuhakikisha Yanga wanalitetea kombe hilo.
Yanga wamezawadiwa dola 30,000, Azam wao wamepata dola 20,000 na Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo walioifunga APR ya Rwanda 2-1 kwenye mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu, wameondoka na dola 10,000.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia huku wakiwa na Kombe la Kagame, baada ya kutawazwa tena kuwa wafalme wa michuano ya soka ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kwa kuibwaga Azam FC mabao 2-0.
Kocha Mkuu wa Yanga, Tom akiungana na wachezaji kushangilia ubingwa huo
 Mashabiki wakiungana na wachezaji wa Yanga kushangilia ubingwa huo
Ubao ulivyokuwa unaonekana baada fainali hiyo kumalizika
Wachezaji wa timu ya Yanga wakishangilia na kombe lao walilokabidhiwa leo mara baada ya kuifunga timu ya Azam FC katika mchezo uliokuwa ni wa kuvutia kwa timu zote baada ya kuitandika timu ya Azam magoli 2-0 kwenye mchezo wa fainali katika michuano ya kombe la Kagame iliyomalizika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Fullshangweblog na kikosi chake cha kazi inawapa hongera Wachezaji wa timu ya Yanga Uongozi na mashabiki wote wa Yanga pamoja na wanachama kwa kuutwaa ubingwa huo kwa mara ya pili mfurulizo hongereni sana.
Wachezaji wa timu ya Azam ambayo imechukua nafasi ya pili wakipita jukwaani na kupewa medali zao baada ya mchezo huo kumalizika jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa.
Wachezaji wa timu ya Vita kutoka DRC Congo wakipta jukwaani na kupokea medali zao Vita wamechukua nafasi ya tau baada ya kuifunga timu ya APR ya Rwanda katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu uliofanyika kalba ya mchezo wa fainali.
Kipre Cheche kulia Mchezaji wa timu ya Azam FC akikokota mpira mbelea ya beki wa Yanga Nidir Haroub Canavaro wakati wa mchezo wa fainali ya kombe la Kagame inayofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii, mpira umekwisha na timu ya Yanga imefanikiwa kutetea kombe la Kagame kwa mara ya pili mfurulizo baada ya kuitandika timu ya Azam FC goli 2-0 jioni hii.
Mashabiki wa timu ya Yanga wakishangilia mara baada ya timu yao kupata goli la kuongoza katika mchezo huo.
Mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Yanga na Azam FC pamoja na maafisa wa CECAFA na wachezaji wa timu zote m,bili.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam akielekea kukagua timu kabla ya mchezo huo kuanza kulia ni , Crecentius Magori kushoto Makamu Mwenyekiti wa timu ya Yanga Clement Sanga na katikati ni Mwenyekiti wa Azam FC mzee Mohamed Said
Timu zikiingia uwanjani kuanzaq mpambano huo.

No comments:

Post a Comment