BUKOBA SPORTS

Monday, July 9, 2012

WENGER:SITABADILIKA, NITANUNUA WACHEZAJI NA KUTUMIA CHIPUKIZI

Arsene Wenger amesisitiza kuwa hatabadili falsafa yake ya muda wote aliokuwa Arsenal ya kununua Wachezaji kwa bei poa na kuwakuza Chipukizi licha ya msimamo huo kuzua mtafaruku mkubwa kwa Wadau wengi wa Klabu yake Arsenal.
Wenger amedai imani yake hiyo ni sawa na ile ya Nguli wa Holland Johan Cruyff ambae aliitumia kwa mafanikio makubwa wakati akiwa Bosi wa Klabu za Ajax Amsterdam na FC Barcelona ambako alivuna Wachezaji wake wa Timu za Kwanza kutoka kwenye Vyuo vya Soka vya Chipukizi kwenye Klabu hizo.
Wenger amesema atatumia falsafa hiyo hiyo ya kufundisha Chipukizi na pia kutumia Wasaka Vipaji wake kutafuta Chipukizi wa kuwakuza Kisoka huku akidai hilo ndilo litailetea Arsenal mafanikio hapo baadae.
Wenger amesisitiza: “Nakubaliana moja kwa moja na Cruyff na mie sitabadilika!”
Alitamka: “Nilikuwa na nafasi mara 10 ya kuondoka kwenda Klabu nyingine lakini sikufanya hivyo kwa sababu nimefanya kazi na dira na falsafa hiyo hiyo nikiwa Arsenal kwa Miaka 16, sintabadilika!”
Alisisitiza: “Kitu cha kusikitisha ni kuwa wakati mwingine kazi yetu inabomolewa na wengine. Unataka kuona Mchezaji akikomaa na kufikia upeo wake wa ubora kwenye Klabu yako. Lakini hilo halitokei! ”
Alisikitika: “Mie naonewa kwa hilo. Nimewapoteza Samir Nasri, Gael Clichy na Cesc Fabregas katika umri ambao wangeweza kucheza Soka lao bora wakiwa Arsenal. Lakini mie sikuhama Klabu wakati ningeweza!”
Kwa msisitizo, Wenger amesema: “Kwa namna hiyo hiyo Watu kama Cruyff hawapotezi nguvu zao kujenga Timu bora kwa kutumia Vijana kwa ajili ya pesa tu. Sote tunafanya hili kwa sababu tunataka Soka inufaike, si kupata fedha tu! ”

No comments:

Post a Comment