BUKOBA SPORTS

Wednesday, August 22, 2012

BARCLAYS PREMIER LEAGUE: CHELSEA V READING LEO SAA 3:45 USIKU STAMFORD BRIDGE

Mechi hii ya Barclays Premier League, BPL, awali ilikuwa ichezwe Septemba 1 lakini imebadilishwa ili kuipisha Chelsea, ambao ndio Mabingwa wa Ulaya, kucheza Fainali ya UEFA Super Cup dhidi ya Mabingwa wa EUROPA LIGI, Atletico Madrid, hapo Agosti 31 huko Monaco.
Jumapili iliyopita, Chelsea wakicheza Mechi yao ya kwanza ya Ligi na kuifunga Wigan huko Uwanja iliyopita, Mchezaji wao mpya Eden Hazard aling’ara na kutengeneza Bao zao zote mbili dani ya Dakika 7 za kwanza na leo anategemewa tena kuwasha cheche zake.
Ingawa Wadau wengi wanategemea Chelsea kuifunga Reading, lakini Wachezaji wa Reading wametamka kuwa wao hawaihofii Chelsea.
Hali za Wachezaji
Kiungo wa Chelsea Ramires huenda akacheza leo baada ya kupona ugonjwa ambao ulimweka nje kwenye Mechi ya kwanza ya Ligi walipoifunga Wigan Bao 2-0 huko Uwanja wa DW.
Lakini, Chelsea itaendelea kumkosa Mchezaji wao mpya Marko Marin ambae ana matatizo ya musuli.
Reading itawakosa Kiungo Jem Karacan, ambae ni majeruhi, Straika Jason Roberts, kifungoni, na Jimmy Kebe, matatizo ya musuli lakini Kipa wao mpya, Stuart Taylor, huenda akachezeshwa.
Uso kwa Uso
•Chelsea hawajawahi kufungwa na Reading kwenye Uwanja wa Stamford Bridge na wameshinda Mechi 3 na kutoka sare 3.
•Mara ya mwisho kwa Reading kuifunga Chelsea kwenye Uwanja wao wa nyumbani ilikuwa kwenye Ligi ya Daraja la Pili Mwezi Machi Mwaka 1930 walipopata ushindi wa Bao 3-1.
RATIBA
Jumatano Agosti 22
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Chelsea v Reading
Jumamosi Agosti 25
[Saa 8 Dak 45 Mchana]
Swansea City v West Ham United
[Saa 11 Jioni]
Aston Villa  v  Everton
Manchester United v Fulham
Norwich City v Queens Park Rangers
Southampton v Wigan Athletic
Sunderland v Reading
Tottenham Hotspur v West Bromwich Albion
[Saa 1 na Nusu Usiku]
Chelsea v  Newcastle United
Jumapili Agosti 26
[Saa 9 na Nusu Mchana]
Stoke City v Arsenal
[Saa 12 Jioni]
Liverpool v Manchester City

No comments:

Post a Comment