BOLT, BLAKE WAENDELEZA UBABE DIAMOND LEAGUE.
Wanariadha bora kabisa duniani kwasasa kutokea nchini Jamaica Usain Bolt na Yohan Blake jana wameendeleza ubabe katika mashindano ya Diamond league yanayoendelea mjini Lausanne, Switzerland baada ya Bolt kushinda mita 200 kwa sekunde 19:58, na Blake mita 100 kwa sekunde 9:95.
Wanariadha hao ambao hawakupambana wenyewe kama ilivyokuwa katika mashindano ya Olimpiki wameonekana kushirikiana kwa karibu, na kwa mujibu wa meneja wa Blake Cubee Seegobin ni sababu za kibiashara zaidi.
No comments:
Post a Comment