Kocha mkuu wa Manchester united Sir Alex Ferguson amethibitisha nia yake ya kuachia ngazi kuifundisha klabu ya Manchester baada ya miaka miwili ijayo baada ya kutngeneza kikosi imara cha msimu huu kinachoundwa na safu imara ya ushambuliaji ya Wayne rooney na Robin Van pesrie ambaye ametua old trafford kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 24 mwisho wa wiki iliyopita.
Kocha huyo mkongwe ambaye anaanza mwaka wake wa 28 akiwa kocha wa united ataanza harakati zake za kuwania taji la ligi ya uingereza msimu huu kwa kupambana na Everton pambano litakalopigwa hapo kesho usiku.
Kocha huyo ana imani na familia ya Glazer katika nia yake ya kutaka kumjumuisha katika kikosi chake beki wa kushoto Leighton Bannes kutoka klabu ya evrton kabla dirisha la usajili halijafungwa hapo tarehe 31,august 2012.
Ferguson mwenye umri wa miaka 70 sasa alichukua jukumu yeye mwenyewe la kumsajili mchezaji Robin van persie kutoka katika klabu ya Arsenal kwa kuongea na Arsene wenger kuhusu suala la uhamisho la mchezaji huyo katika nia yake ya kuhakikisha kwamba msimu huu anarudisha taji ambalo alilipoteza kwa manchester city msimu uliopita.
WAKATI HUO HUO NAYE ALEXANDER BUTTNER KUTUA OLD TRAFFORD KUPIMA AFYA
LEO Alexander Buttner amesafiri kutoka Schipol Airport huko Amsterdam kwenda Manchester ili kupima afya yake na kukamilisha Uhamisho wake kutoka Klabu ya Vitesse Arnhem ya Holland kwenda Manchester United.
Buttner, Miaka 23, ni Fulbeki wa kushoto ambae hivi karibuni amekuwa akiwindwa na Southampton, Fulham na Queens Park Rangers.
Akisimulia Uhamisho wake huu ambao utagharimu Euro Milioni 5, Buttner amesema: “Kama Wiki moja iliopita ungeniambia ntakuwa nikicheza pamoja na Robin van Persie ndani ya Manchester United, ningekupeleka moja kwa moja Hospitali ya Wenda wazimu!”
Aliongeza: “Mwezi mmoja uliopita, Manchester United ilituma Barua pepe ikionyesha nia yao kunichukua lakini katika Siku 4 zilizopita mambo yalikamilika. Sijaongea na Sir Alex Ferguson lakini mambo yakienda sawa itatokea tu.”
Buttner amekuwa na mgogoro na Klabu yake Vitesse Arnhem kuhusu hatima yake ya baadae na alikuwa amezuiwa kufanya mazoezi na Timu ya Kwanza huku suala lake likiwa mbele ya Vyombo vya Usuluhisho na mwenyewe amesema: “Kwa kuzuiwa kucheza na Timu ya Kwanza na Kesi yangu dhidi ya Vitesse Arnhem ikiwa kwenye Vyombo vya Sheria, Uhamisho huu ni zawadi nzuri kwangu!”
Manchester United wamekuwa wakisaka Fulbeki wa kushoto ili kumsaidia Patrice Evra kwenye nafasi hiyo baada ya mbadala wake, Fabio da Silva, kupelekwa QPR kwa mkopo.
No comments:
Post a Comment