Tottenham imetangaza kuwa wamekubali Uhamisho wa Kiungo wao Luka Modric kwenda Real Madrid kwa Ada inayokisiwa kuwa ni Pauni Milioni 30 na hivyo kumaliza mvutano wa muda mrefu kati ya Mchezaji huyo na Klabu yake.
Uthibitisho wa Uhamisho wa Mchezaji huyo wa Kimataifa kutoka Croatia umetolewa kwenye Tovuti ya Tottenham ambako Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Daniel Levy, ametoa shukrani kwa Modric na kusema hawakutaka kumuuza ili imebidi tu.
Habari hizi pia zimethibitishwa na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, ambae ameelezea furaha yake na kumkaribisha Modric huko Madrid.Mbali ya makubaliano ya Uhamisho huu wa Modric, Klabu hizo mbili pia zimetiliana saini Mkataba wa kuanzisha Ushirika kati yao utakaohusisha Wachezaji, Makocha na Biashara.Luka Modric alihamia Spurs Mwaka 2008 kutoka Dinamo Zagreb na kuichezea Spurs Mechi 160 na kufunga Mabao 17.
KUHUSU LUKA MODRIC
Luka Modrić is a Croatian footballer who plays for Real Madrid and for the Croatia national football team as a midfielder. Modrić's childhood coincided with the Croatian War of Independence.
KIMO: 1.75 m
UZITO: 67 kg
NAFASI: Midfielder
Spouse: Vanja Bosnic (m. 2011)
MSHAHARA: Euro 5,600,000 (2012)
No comments:
Post a Comment