BUKOBA SPORTS

Friday, August 10, 2012

KIRAFIKI: BARCELONA V MAN UNITED WATOKA SARE DAKIKA 90 - BARCA YASHINDA KWA PENATI 2-0

Kwenye Mechi ya Kirafiki iliyochezwa Uwanja wa Ullevi huko Gothenburg, Sweden, Manchester United na Barcelona zilitoka sare ya 0-0 katika Dakika 90 lakini Barcelona wakashinda kwa Mikwaju ya Penati 2-0 ambazo ziliamuliwa kabla ziwe 3 tu na Man United kukosa zote 2 za kwanza na Barca kufunga zao zote mbili za kwanza.
Ndani ya Dakika 90, Man United walipoteza nafasi safi ya kufunga bao baada ya kupewa Penati katika Dakika ya 45 kufuatia Nani kuchezewa faulo na Cristian Tello lakini mkwaju wa Wayne Rooney ukaokolewa na Kipa Valdes na kumrudia tena Rooney aliepiga nje.
Kwenye Mikwaju ya hizo Penati 3, kwa Man United Nani alipiga posti ya juu na ya Ashley Young iliokolewa na Kipa Pinto alieingia badala ya Valdes na kwa Barca Xavi na Gerard Pique walifunga.
Deja vu: Ashley Young failed to score from the penalty spot for Manchester United just weeks after missing for England at Euro 2012 (below)
 Ashley Young failed to score from the penalty spot for Manchester United

Miss: Ashley Young hits the cross bar during the penalty shoot-out between England and Italy
Ashley Young alikosa penati hapa...anabalaa gani? huyu Young... na kwenye EURO alichemka..
VIKOSI
Man United: De Gea; Valencia, Vidic, Ferdinand, Evra; Nani, Anderson, Scholes, Young; Rooney, Welbeck
Akiba: Lindegaard, Berbatov, Hernandez, Carrick, Powell, Kagawa, Macheda, Wootton, Brady, M Keane, Lingard
Barcelona: Valdes; Alves, Puyol, Mascherano, Adriano; Roberto, Busquets, Iniesta; Sanchez, Messi, Tello
Akiba: Pinto, Pique, Fabregas, Xavi, Villa, Bartra, Rodriguez, Alba, Montoya, Afellay, Fontas, Sanchez, Rafinha

No comments:

Post a Comment