Timu ya Manchester City wamefanikiwa kumsajili mchezaji ambaye kwa miaka mingi alikuwa akisemekana atasajiliwa na Man United lakini habari imegeuka na leo hatimaye amesajili Manchester lakini sio United ila ni majirani wao City.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akisifiwa kwa uwezo wake wa uwanjani tokea alipoanza chezea timu ya wakubwa ya Everton.
Taarifa toka katika mtandao wa Everton imesema,
“Everton wamekubaliana na Man City kuhusiana na usajili wa Jack Rodwell.
Mchezaji huyo anatarajiwa fanyiwa vipimo vya afya jumapili kwa ajili ya kujiunga na Man City.” Timu ya Manchester City wamefanikiwa kumsajili mchezaji ambaye kwa miaka mingi alikuwa akisemekana atasajiliwa na Man United lakini habari imegeuka na leo hatimaye amesajili Manchester lakini sio United ila ni majirani wao City.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akisifiwa kwa uwezo wake wa uwanjani tokea alipoanza chezea timu ya wakubwa ya Everton.
Rodwell atajiunga na Man City timu ambayo tayari inaviungo vya kutosha wakiwemo akina Gareth Barry, Nigel de Jong na Yaya Toure.
Man City wanata kuwa na wachezaji wengi waingereza ili kuweza fikia sheria mpya ya Premier League ya kila timu kuwa na idadi maalum ya wacheza wa Uingereza. Baada ya Usajili huo Mancini anataka hamisha nguvu zake katika usajili wa mchezaji wa Swansea Scott Sinclair.
No comments:
Post a Comment