BUKOBA SPORTS

Thursday, August 30, 2012

MASTAA KUMI WA SOKA WANAOONGOZA KWA KULIPWA MISHAHARA MIKUBWA, NA MALI ZAO!



Hii ndio nyumba ya Lionel Messi iliyoko Barcelona, stori kwa mujibu wa barcainfo.
Kwa mara nyingine tena Lionel Messi anatengeza kichwa cha habari baada ya kutwajwa kuwa mwanasoka anayelipwa mkwanja mrefu kuliko wote duniani, huku David Beckham akishika nafasi ya pili na Cristiano Ronaldo akishika nafasi ya tatu.
Kutokana na ripoti iliyotolewa na jarida la France Football ambayo imetoka leo, mshambuliaji huyo wa Barcelona anaingiza Pound 33 million kwa mwaka kupitia mishahara na fedha za matangazo wakati LA Galaxy midfielder na mchezaji wa zamani wa Manchester United David Beckham ambaye amekuwa akiongoza kwa muda mrefu listi hii, amekuwa wa pili akiingiza pound milioni 31.5, wakati star wa Real Madrid Ronaldo akikusanya pound milioni 29.2 ndani ya mwaka mmoja uliopita.

Samuel Eto’o nae yupo katika nafasi ya nne akiingiza pound milioni 23.3m huku Wayne Rooney akikamata nafasi ya tano na pound milioni 20.6.

Beckham ndani ya Rolls Royce....

Beckham akiwa mitaani Marekani na watoto wake, kwenye hii picha anaonekana kamkodolea macho yule mrembo pale pembeni....

Hii ni moja kati ya majumba ya kifahari ya Christiano Ronaldo anaeichezea Real Madrid.

Hawa jamaa hawamiliki gari moja au nyumba moja... hizi ni baadhi tu ya mali wanazomiliki......


Bwana Samuel Eto.

Bwana Wyne Rooney.

Wyne Rooney ndio muhusika wa hii kwa mujibu wa world football extra.

Yaya Ture wa Man City.

Fernando Torres baada ya kusimamishwa na polisi.

Hii ndio AUDI ya Fernando Torres, akiwa kifamilia zaidi.......DUhhhhhh!!! jamani eeeh

Hata kama hajafunga goli kwenye mechi 25 mambo yake ni super sana, nadhani unamuona hapo ndani ya hicho kitu cheusi cha Aston Martin.

Nyumbani kwa Fernando.



Sebleni kwa Fernando Torres.

Kwa mujibu wa Soccer Magazine, hii ndio nyumba ya mchezaji Kaka wa Real Madrid ni nyumba ya 7.2 million euros na ipo mita 400 kutoka kwenye nyumba ya mchezaji mwenzake wa Real Madrid Cristiano Ronaldo sehemu inaitwa ozuelo de Alarcón, Madrid.

Hii ndio list ya wachezaji wengine wanaoongoza kwa kulipwa pesa ndefu. kumbuka hii ilichukuliwa muda mrefu kidogo kwa sasa wenda kukawa kuna mabadiliko au la!

No comments:

Post a Comment