Katika Mechi ya kwanza ya kugombea Supercopa iliyochezwa Nou Camp Alhamisi Usiku, kumeifanya Mechi ya marudio ya kugombea Kombe hili itakayochezwa Jumatano ijayo Agosti 29 iwe Mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa na Wadau wa Soka Duniani kote.Hii ilikuwa ‘El Clasico’ ya kwanza kwa Meneja mpya wa Barca, Tito Vilanova, na ametoka mbabe lakini bila shaka ipo kazi kubwa katika Mechi ya maruduano.
Ronaldo akishangilia mara baada ya kufunga goli dk ya 55
Xavi (katikati) akifurahia na wenzake
Ronaldo ndie aliefunga bao la kwanza kwa Real kwa kichwa kufuatia kona ya Ozil lakini Barca walisawazisha Dakika moja baadae kwa bao la Pedro ambae alipokea ndefu kutoka kwa Mascherano mara tu baada ya mpira kuwekwa kati baada ya Barca kufungwa.
Bao la pili la Barca lilifungwa kwa Penati ya Lionel Messi baada ya Iniesta kuangushwa na Ramos ndani ya boksi na Barca wakapiga bao la 3 kupitia Xavi.
Messi akijaribu kumpita Sami Khadira jana usiku Camp Nou
Jose Mourinho na Francesc 'Tito' Vilanova wakipongezana kwa kupeana mikono
Ronaldo akijaribu kupita kwenye ngome ya Barcelona
Messi ... hapa upiti ndugu yangu tulia Fabio Coentrao
Lakini zikiwa zimesalia Dakika 5 mpira kwisha Kipa wa Barca Valdes alifanya makosa makubwa pale aliporudishiwa mpira na kujaribu utaalam wa kumzunguka Angel Di Maria lakini Mchezaji huyo wa Real akaunasa mpira na kufunga.
MAGOLI
Barcelona
56 Pedro
70 Messi
78 Xavi
Real Madrid
55 Ronaldo
85 Angel Di Maria
MAGOLI
Barcelona
56 Pedro
70 Messi
78 Xavi
Real Madrid
55 Ronaldo
85 Angel Di Maria
VIKOSI
Real Madrid: Casillas, Arbeloa, Albiol, Sergio Ramos, Coentrao, Alonso, Khedira, Callejon, Ozil, Ronaldo, Benzema
Akiba: Varane, Granero, Marcelo, Adan, Higuain, Di Maria, Lass Diarra, Nacho, Morata, Jesus
Barcelona: Valdes, Alves, Pique, Mascherano, Adriano, Busquets, Xavi, Iniesta, Alexis, Messi, Pedro
Akiba: Fabregas, Puyol, Villa, Pinto, Jordi Alba, Sergi Roberto, Tello
No comments:
Post a Comment